Translate

Jumamosi, 27 Aprili 2019

Hukmu ya Jimai mchana wa Mwezi wa Ramadhaan

Swali

Assalaamu alaykum..nilikuwa naomba kuuliza ..wanandoa wanaojimai mchana wa ramadhan wameekewa adhab mbalimbal za kufanya mf kufunga miez miwil mfululizo.
Je hukumu hii wataitekeleza mke na mume au itamhusu mmoja wao

Majibu

Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh

Naam Shukrani kwa Swali lako ndugu yangu katika Imaani.

Ikiwa ni wakati wa Swawm basi ni haraam na dhambi kubwa na kafara (malipo) yake ipo katika Hukmu za Namna Tatu.

1.Hukmu ya Kwanza  ni kuachia huru mtumwa

2.Hukmu ya Pili kama hamtoweza  basi mfunge miezi miwili mfululizo (bila ya kukatiza).

3.Hukmu ya Tatu ikiwa hamtoweza kufanya hivyo basi mlishe masikini 60 au watu wanaohitaji.

Angalizo

Kufanya hivyo inawapasa wote wawili mume na mke kila mmoja afanye sehemu yake.

Lakini kama mke alilazimishwa kufanya kitendo hicho basi yeye haimpasi kulipa 'kafara'.

Ama kwa kuongezea ni kwamba ikiwa baada ya kufuturu, hakuna shaka kuwa imeruhusiwa.

Hii ni kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

((أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَى نِسَآئِكُمْ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ عَلِمَ اللّهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ فَالآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُواْ مَا كَتَبَ اللّهُ لَكُمْ وَكُلُواْ وَاشْرَبُواْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّواْ الصِّيَامَ إِلَى الَّليْلِ وَلاَ تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ تِلْكَ حُدُودُ اللّهِ فَلاَ تَقْرَبُوهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللّهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ))

((Mmehalalishiwa usiku wa Swawm kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo Amekukubalieni toba yenu na Amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni Aliyokuandikieni Allaah. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka Allaah, basi msiikaribie. Namna hivi Allaah Anabainisha Ishara Zake kwa watu ili wapate kumcha)) [Al-Baqarah: 187]

Kabla ya kuteremshwa Aayah hizo Maswahaba walikuwa wakijizuia kuonana na wake zao nyakati za usiku za Ramadhaan.

Ilikuwa wameruhusiwa kula na kunywa na kujimai kutoka mwanzo wa Magharibi baada ya kufuturu hadi wakati wa 'Ishaa pekee.

Wale waliolala kabla ya 'Ishaa au walioswali Swalah ya 'Ishaa hawakuruhusiwa kunywa au kula au kujimai hadi usiku wa siku ya pili yake.

Hivyo waliliona ni jambo gumu na hadi baadhi ya Maswahaba walishindwa kuvumilia wakaingia kufanya jimai. Ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akalifanya liwe jepesi kwa Rahma Yake.

Ruhusa ya kujimai hivyo ipo kuanzia baada ya kufuturu hadi kabla ya Alfajiri kuingia kama ilivyotajwa katika hizo Aayah ((Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku…))

Na Allaah anajua zaidi.

Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*



http://bit.ly/2IW8sOO i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...