Swali
Swali langu ndugu zangu katka iman ..inakuaje binti waislam anaishina mkristu na amezaa nae watt zaidi ya mmoja alafu anajiweka katk kuufunga mwezi waradhani nabado anaendelea kuishi nae na anahudumiwa kama mke
Je hukumu yake nini au je inaswihi au laa
Jibu
Naam Swawm yake inaswihi
Naam kwanza kabisa ni WAJIBU kwa Muislam kufunga Mwezi wa Ramadhaan.
Maulamaa wamekubaliana kufunga ni wajibu kwa Muislam mwenye akili timamu, Baleghe, mwenye afya na mkazi wa mji. Tukiongezea wanawake waliotwaharika na hedhi na nifasi.
Kwahiyo ikiwa wewe Mwanamke ni Muislam basi ni Lazima Ufunge Mwezi wa Ramadhaan na haijalishi unaishi na kafiri.
Jambo lingine ni kwamba ni HARAMU kwa Mwanamke wa Kiislamu kuishi na Mwanaume Mkristo kama Mumewe.
Hapo Mwanamke unakuwa unafanya Zinaa na Allaah amekataza Zinaa na ni Uchafu.
Allaah(Subhaana wa Taala) Ametoa ruhusa kwa mwanamume wa Kiislamu tu kumuoa mwanamke wa Kitabu (Mkristo au Myahudi).
Hata hivyo Allaah (Subhaana wa Taala) hakuliacha jambo hilo bila kuliekea masharti.
Ikiwa masharti hayo yaliyowekwa yatakuwa ni yenye kutimizwa basi kutakuwa hakuna tatizo. Aayah inayohusiana na hilo ni ile ya Suratul Maa’idah Aya ya 5
*“Leo mmehalalishiwa vyote vizuri, na pia chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao. Na wanawake Waumini Muhswanaat na wale Muhswanaat waliopewa Kitabu kabla yenu ikiwa mtawapatia ujira (mahari) wao kuwataka kwa ndoa wala sio kuweka wazi zinaa wala kuwachukua kama vimada kwa siri”.*
Ama hili neno *Muhswanaat* lina maana ya *wanawake wema watwaharifu waliojiweka mbali na uzinzi(Uzinifu).*
Na ibara za mbele zinamaanisha kuwa wanawake hawa wasiwe ni wale wenye kufanya zinaa kwa siri au dhahiri.
Basi ikiwa Mkristo ana sifa hizo basi unaweza kumuoa baada ya kutimiza na hayo masharti mengine ya ndoa.
Hukumu ya zinaa ikiwa ni kwa siri au ni dhahiri adhabu yake ni mijeledi 100 ikiwa mwanamke au mwanamume hajaolewa na ikiwa ameoa au ameolewa basi adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka kufa.
Kwahiyo Kinachotakiwa Hapo Mwanamke wa Kiislamu ni kuachana kabisa na huyo Mwanaume Mkristo na Kisha Kufanya Tawbah ya Kweli.
Ama pia huyo mwanaume anaweza kubadili Dini na kusilimu kuwa Muislam na Kisha kufunga Ndoa ya Kisheria.
Hukmu ya Watoto watakuwa ni wa mama kwasababu watoto wamepatikana kwa njia ya Zinaa.
Ama Kuhusu Swawm ikiwa Mwanamke atafunga basi Swawm yake Itaswihi.
Naam mara nyingi sisi kama wanadamu na hasa kama waislamu tunakosa hisia kwa kuona kuwa tukifanya dhambi kwa siri basi huwa hakuna dhambi wala adhabu.
Allaah (Subhaana wa Taala) Anasema:
((كَذَلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ))
((Namna hivi inakuwa adhabu (Ya Mola duniani) Na adhabu Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangalijua!))
[Surat Al-Qalam Aya ya 33]
Nasaha zangu nasaha tunawausia ndugu na dada zetu sote kwa pamoja tumche Allaah kwani mafanikio yetu hapa duniani na kesho Akhera ni kuwa katika msimamo huo.
Ikiwa tumefanya jambo baya, la makosa hiyo ni katika udhaifu wetu, binadamu. Hivyo, tuombe toba na tufanye mambo mema. Na tunamuomba Allaah Atuepushe kufanya madhambi kwa siri au dhahiri.
Na Allaah Anajua zaidi.
http://bit.ly/2ISsURM i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni