- Tia nia, jitahidi na omba dua kwa wingi, Allah (swt) akujaalie Ramadhan yenye mafanikio.
- Panga siku yako, kila siku katika mwezi wa Ramadhani. Jitahidi kufanya hivyo usiku kabla siku haijaanza. Chagua mambo matatu muhimu unayotaka kuyakamilisha siku ijayo na uyaandike katika mipango yako.
- Usikose daku (suhur) hata siku moja. Amka saa moja kabla ya Alfajiri na ule chakula cha kutosha na kilicho bora.
- Anza kufanya mambo yaliyo muhimu zaidi asubuhi na mapema, baada ya swala ya alfajiri na ujitahidi kumaliza jambo moja au mawili.
- Jitahidi kulala kidogo mchana kabla au baada ya dhuhr, ila sio zaidi ya dakika 20.
- Fanya mipango yako kwa kuzingatia wakati wa swala, na si kinyume chake.
- Tenga angalau saa moja kwa ajili ya kusoma Qur’an kila siku.
- Futuru kwa tende na maziwa au tende na maji, nenda kaswali kisha rudi na ule mlo mwepesi.
- Toa sadaka kwa wingi. Jihusishe katika kuandaa futari, kujitolea na kuwasaidia mayatima n.k. Pata thawabu kwa kuwatumikie wengine
- Usiache fursa ya kufanya da’wah! Mtu akikuuliza kwanini hauli, wape maelezo mazuri kuhusu Ramadhani na Uislamu.
Ili kusoma kwa kingereza, bonyeza hapa
from TIF http://bit.ly/2GDDFDW
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni