Yanayomlazimu Mtu Mzima na Mwenye Ugonjwa wa kuendelea
Asioweza kufunga, kwa ajili ya utu uzima au kwa ajili sababu nyenginezo, hatofunga badili yake atalisha maskini mmoja kwa kila siku aliokosa kufunga. Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Amesema:
وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ
“Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).” (Suuratul Baqarah 02 : 184)
‘Atwaa’ amesema alimsikiya Ibn ´Abbaas akisoma Aayah hii kisha akasema ‘’Haikuondolewa. Inawahusu watu wazima waume kwa wake ambao hawawezi kufunga. Ndio watalisha masikini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga.” [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl na.912 na Imerikodiwa na Imaam Al-Bukhaariy].
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2J1xJao i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni