Mambo yanayofaa Kufanywa na Mwenye Kufunga
1. Anaruhusiwa kujisuuza kichwa na maji ya baridi.
2. Kusukutua na maji bila kuyamiza na kutiya maji puani bila kuingiya ndani ya mwili.
3. Kuumikwa ama kutoa damu kwa ajili ya matibabu.
4. Kumbusu au kumgusa mke wako bila matamanio kwa mwenye kuweza kujizuwiya.
5. Mwenye kuamka asubuhi na akiwa katika janaba.
6. Kuchelewesha kufungua swawm mpaka saa ya kula daku.
7. Kutumia mswaki, manukato, wanja, dawa ya macho na kudungwa sindano kwa ajili ya matibabu.
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2J1tNqa i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni