Kila amali njema atendayo Muislamu inalipwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mara kumi yake ikiwemo Swawm kama ilivyothibiti katika Hadiyth zifuatazo:
عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ))
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): ((Kila ‘amali njema ya mwana Aadam inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa] [Muslim na Ahmad]
Na pia:
عَنْ أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayefunga (Swawm) kila mwezi siku tatu, ni sawa na Swawm ya milele)) Kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: “Atakayekuja kwa 'amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo.” Siku moja kwa malipo ya siku kumi. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Suwrat Al-An’aam (160)]
Miongoni mwa Swiyaam za Sunnah ni Swiyaam za Ayyaamul-Biydhw kwa dalili ya Hadiyth:
عَنْ جريرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَن النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ صِيَامُ الدَّهْرِ، أَيَّامُ الْبِيضِ صَبِيحَةَ ثَلاثَ عَشَرَةَ وَأَرْبَعَ عَشَرَةَ وَخَمْسَ عشَرَةَ))
Imepokelewa kutoka kwa Jariyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam siku tatu kila mwezi ni sawa na swiyaam ya milele; na masiku meupe ni tarehe kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano [13, 14, 15])) [An-Nasaaiy (2420) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb(1040)]
Maana Ya Al-Biydhw: Masiku hayo yameitwa ‘Al-Biydhw’ (meupe) sababu usiku wa siku hizo hung'aa kutokana na mwanga wa mwezi. Ayyaam Al-Biydhw (Masiku Meupe) tarehe zake ni 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa kalenda ya Kiislamu.
Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasisitiza kufunga Swiyaam siku tatu katika kila mwezi, ikiwa ni Ayyaamul-biydhw au Jamatatu na Alkhamiys au siku zozote zile katika mwezi:
عن أبي ذر رضي الله عنه: قال لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((يَا أَبَا ذَرٍّ، إِذَا صُمْتَ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَصُمْ ثَلاثَةَ عَشَرَ وَأَرْبَعَةَ عَشَرَ وَخَمْسَةَ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Ee Abuu Dharr! Endapo utafunga (Swawm) siku tatu za kila mwezi, basi funga siku ya 13, ya 14, na ya 15)) [Imepokewa na At-Tirmidhiy na kasema Al-Albaaniy kuwa ni Swahiyh]
Na pia:
قال صلى الله عليه وسلم: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ بِمَا يُذْهِبُ وَحَرَ الصَّدْرِ صَوْمُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْر))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je, nikujulisheni jambo litakaloondosha uovu wa moyo? Ni kufunga (Swawm) siku tatu kila mwezi)) [An-Nasaaiy (2/2386) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy(2249)]
Asw-Suyuutwiy (Rahimahu Allaah) amesema katika An-Nihaayah: “Uovu wa moyo ni; udanganyifu, wasiwasi, na imesemwa pia ni uhasidi, chuki, na imesemwa pia uadui na imesemwa ghadhabu”
Fadhila Za Swawm Jumatatu Na Alkhamiys:
عن أبي هريرة رضي الله عنه: تُعرَضُ الأعمالُ يومَ الاثنينِ والخميسِ فأحبُّ أن يُعرَضَ عملي وأنا صائمٌ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Amali zinapandishwa siku ya Jumatatu na Alkhamiys, basi napenda kwamba zipandishwe 'amali zangu nikiwa mimi nina Swawm.” [Swahiyh At-Tirmidhiy 747, Swahiyh At-Targhiyb 1041]
Na kuhusu Swiyaam ya Jumatatu:
عَنْ أَبِي قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنْ صَوْمِ الِاثْنَيْنِ فَقَالَ: ((فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَيَّ)).
Kutoka kwa Abuu Qataadah Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu Swawm ya Jumatatu akasema: “Nimezaliwa siku hiyo na siku hiyo nimeteremshiwa (Qur-aan).” [Muslim]
Baadhi ya fadhila nyinginezo za Swawm:
1. Kufunga (Swawm) ni kuepushwa na moto masafa ya miaka sabini.
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: مَنْ صَامَ يَوْماً فِي سَبِيلِ اللَّهِ بَعَّدَ اللَّهُ وَجْهَهُ عَنْ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا .
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefunga Swawm siku moja kwa ajili ya Allaah, Allaah Atamweka mbali uso wake na moto masafa ya miaka sabini)) [Muslim 2/208]
Na katika Hadiyth nyingine pia:
عن جابر رضِي الله عنه عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قال: ((الصِّيام جُنَّة يَستَجِنُّ بها العبدُ من النار))
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam ni kinga itamuokoa mja kutokana na moto [wa Siku ya Qiyaamah])) [Ahmad 2/402, Swahiyh At-Targhiyb 1/411 na Swahiyh Al-Jaami’ 3880]
2. Mwenye kufunga (Swawm) atafunguliwa mlango wa Rayyaan huko Jannah.
عَنْ سَهْلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ فِي الْجَنَّةِ بَابًا يُقَالُ لَهُ الرَّيَّانُ يَدْخُلُ مِنْهُ الصَّائِمُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ يُقَالُ أَيْنَ الصَّائِمُونَ فَيَقُومُونَ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ فَإِذَا دَخَلُوا أُغْلِقَ فَلَمْ يَدْخُلْ مِنْهُ أَحَدٌ ))
Imepokelewa kutoka kwa Sahl (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika Jannah kuna mlango unaitwa Rayyaan, wataingia humo siku ya Qiyaamah wenye kufunga (Swawm), hatoingia yeyote mwingine. Itasemwa: “Wako wapi waliokuwa wakifunga? Watasimama kuingia hatoingia yeyote mwengine, watakapoingia, utafungwa, basi hatoingia mwengine)) [Al-Bukhaariy 1763, Muslim 1947]
3. Swawm ni kwa ajili ya Allaah Pekee na mwenye Swawm hupata furaha mbili; anapofuturu na atakapokutana na Rabb Wake. Na harufu ya mdomo wake ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk.
عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ فَرْحَةٌ عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفُ فِيهِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ))
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): ((Kila 'amali njema ya mwana Aadam inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa; ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa anayefunga atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Rabb wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliye na Swawm ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk)) [Muslim na Ahmad]
4. Du’aa ya mwenye Swawm inakubaliwa.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ, الإِمَامُ الْعَادِلُ, وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ, وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ ...))
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (([Watu] Watatu hazirudishwi du'aa zao; Imaam muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na du'aa ya aliyedhulumiwa…)) [Ahmad na Ibn Maajah. Pia Al-Bayhaqiy 3/345 na As-Silsilah Asw-Swahiyhah 1797]
5. Swawm itakuombea shafaa-‘ah Siku ya Qiyaamah.
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((الصِّيَامُ وَالْقُرْآنُ يَشْفَعَانِ لِلْعَبْدِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، يَقُولُ الصِّيَامُ: أَيْ رَبِّ مَنَعْتُهُ الطَّعَامَ وَالشَّهَوَاتِ بِالنَّهَارِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ. وَيَقُولُ الْقُرْآنُ: مَنَعْتُهُ النَّوْمَ بِاللَّيْلِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ. قَالَ : فَيُشَفَّعَانِ))
Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin ‘Amr (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam na Qur-aan zitamuombea shafaa’ah mja siku ya Qiyaamah. Swiyaam itasema: “Ee ee Rabb! Nimemzuia chakula chake na matamanio wakati wa mchana, basi nnamuombea shafaa-‘ah.” Na Qur-aan itasema: “Nimemzuia usingizi wake wakati wa usiku basi nnamuombea shafaa-‘ah.” Akasema: ((Basi [viwili hivyo] vinaombea shafaa-‘ah na kukubaliwa]. [Ahmad (174/2) Al-Haakim (1/554), Al-Bayhaqiy (3/181) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaamiy’ 7329]
6. Swawm hakuna mfano wake.
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: مُرْنِي بِأَمْرٍ آخُذُهُ عَنْكَ قَالَ: ((عَلَيْكَ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَا مِثْلَ لَهُ))
Kutoka kwa Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: “Niamrishe jambo [litakalonifaa Aakhirah] nilichukue kwako.” Akasema: ((Shikilia Swawm kwani hakika hakuna mfano wake)) [An-Nasaaiy]
7. Ukifariki ukiwa katika Swawm utaingia Jannah nayo ni Husnul-Khaatimah.
عن حذيفة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قَال: ((مَن خُتِمَ له بصيام يومٍ دخل الجنة))
Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekuwa 'amali yake ya mwisho kabla ya kufariki ni Swiyaam ataingia Jannah)) [Ahmad 5/391. Swahiyh At-Targhiyb 1/412, Swahiyh Al-Jaami’ 6224]
from Muislamu Blog http://bit.ly/2GS7IrF
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni