Swali: 03: Ikiwa katika mkono wangu mmoja au yote miwili nina donda linalodhurika kwa maji – nifanye Tayammum? Je, sehemu zinazopanguswa katika Tayammum ni zilezile kama wakati wa kutia wudhuu´?
Jibu: Ndio, sehemu zinazopanguswa katika Tayammum ni zilezile kama wakati wa kutia wudhuu´. Afute uso wake kwa udongo kuanzia sehemu ya juu ya uso mpaka kwenye ndevu na kuanzia kwenye sikio moja hadi lingine. Apanguse mikono yake kwa nje na kwa ndani mwanzoni mwa vidole mpaka kwenye ncha zake. Mkononi mwake kukiwa kidonda basi inatosha kufuta kwa udongo juu ya kidonda hicho. Ikiwa mkono wake mmoja ni mzima na mwingine ndio uko na kidonda basi ataosha ule mkono mzima na atafuta kwa maji juu ya kile kidonda kama ambavo mikono yake miwili au mkono mmoja utakuwa na plasta au kitu mfano wake. Ikiwa maji yanamdhuru au ni machafu basi itamtosha kufanya Tayammum.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2Wc8hCO
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni