Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad.
Naam, Ndugu zangu katika Imaani Muda huu napenda kuchukua Fursa hii kufikisha kwenu japo kwa Uchache Darsa letu lenye anuani isemeyo Fadhila za Kusuluhisha Waliogombana
➡Anasema Allaah سبحانه وتعالى Kwamba⤵
((لاَّ خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلاَّ مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلاَحٍ بَيْنَ النَّاسِ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ ابْتَغَاء مَرْضَاتِ اللّهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمً ))
((Hakuna kheri katika mengi ya wanayoshauriana kwa siri, isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Allaah basi Tutakuja mpa ujira mkubwa))
↪Suratul An-Nisaa Aya ya 114.
➡Na kasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwamba⤵
((ألا أخبركم بأفضل من درجة الصيام والصلاة والصدقة ؟ إصلاح ذات البين وفساد ذات البين هي الحالقة)) رواه أحمد وأبو داود والترمذي صحيح الجامع
((Je, nikujulisheni lililo na daraja bora kuliko Swawm na Swalah na Sadaqah? Ni kusuluhisha baina ya watu. Na ama kuharibu uhusiano (baina ya watu) ni uharibifu.
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad na Abu Daawuud na At-Tirmidhy katika Swahiyhul-Jaami'i
Ndugu zangu katika Imaani, Katika mambo ya kheri Aliyoyataja Allaah سبحانه وتعالى watu wanapozungumza kwa siri ni kuamrishana kutoa sadaka au kutenda mema. Kisha Ametaja kuhusu kupatanisha watu, jambo ambalo mara kwa mara hutokea katika jamii na khaswa jamii yetu.
➡Na bila ya shaka ugomvi na ikhtilaaf ni katika silaha ya hatari kabisa anayopenda kuitumia Shaytwaan kufarikisha watu watengane na kuchukiana baada ya kuwa ni ndugu au marafiki au majirani au baina ya mume na mke.
➡Lakini Uislamu haukuacha kutilia hima jambo la kusuluhisha ugomvi kwa kutukumbusha fadhila zake kubwa katika Qur-aan na Sunnah kama tunavyoona katika Aayah na Hadiyth hapo juu.
➡Lakini inasikitisha kuona kwamba jambo hili la kusuluhisha halikutiliwa mkazo sana katika jamii yetu, kwani wangapi tunasikia miongoni mwetu kuwa *'fulani kagombana na fulani na hawasemeshani',* kisha zikapita siku na miezi na miaka hawa watu wako katika hali hii jambo ambalo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amekataza kabisa zisipite zaidi ya siku tatu ndugu wa Kiislamu kuwa katika hali kama hiyo⤵
عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه قال : قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( لا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ ، يَلْتَقِيَانِ فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا ، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلامِ .(( رواه البخاري ومسلم و في رواية أبو داود بإسناد على شرط البخاري ومسلم
((فَمَنْ هَجَرَ فَوْقَ ثَلاَثٍ فَمَاتَ دَخَلَ النَارَ ))
Imetoka kwa Abu Ayyuub Al-Answariy رضي الله عنه ambaye alisema: Kasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم: ((Haimpasi Muislamu amhame ndugu yake zaidi ya siku tatu hata wanapokutana huyu anamgeuzia (uso) huyu na huyu anamgeuzia (uso) huyu. Na aliye mbora wao ni yule anayeanza kutoa salaam))
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhariy na Muslim na katika Riwayaah ya Abu Daawuud
Na nyingine...
((Atakayemhama (mwenzake) zaidi ya siku tatu akafariki basi ataingia motoni))
Ndugu zangu katika Imaani,na huenda ikawa kila mmoja anataka kupatana na mwenziwe lakini Shaytwaan amewatia ari kuwa vipi aanze yeye?
➡Na pia pengine huenda wakawa ni ndugu, au jamaa au jirani lakini hakuna mmoja wetu anayekimbilia kusuluhisha, sababu ni kwamba kila mmoja ameshughulika na kazi zake na maisha yake.
➡Kwa hiyo tulichukulie hima jambo hili bila ya kuchelewesha kila inapotokea ugomvi baina ya ndugu wa Kiislamu na kufanya hivyo ni kumcha Allaah سبحانه وتعالى, kumtii Allaah سبحانه وتعالى na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na ndio sifa ya Waumini kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى kwamba⤵
((فَاتَّقُواْ اللّهَ وَأَصْلِحُواْ ذَاتَ بِيْنِكُمْ وَأَطِيعُواْ اللّهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ))
((Basi mcheni Allaah na suluhisheni mambo baina yenu, na mtiini Allaah na Mtume Wake ikiwa nyinyi ni Waumini))
↪Surat Al-Anfaal Aya ya 1
Ndugu zangu katika Imaani, Tukiendelea na fadhila za kusuluhisha waliogombana wakakhasimiana, na iwapo baada ya kusoma mada hii tutazithamini fadhila hizi, basi kila mmoja wetu atakimbilia kufanya hima ya kupatanisha ndugu zetu wa Kiislamu waliogombana /waliokhasimiana.
➡Allaah سبحانه وتعالى Amelichukia jambo hili kwani linavunja asili ya undugu wa Kiislamu kama Anavyosema⤵
((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ))
((Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu))
↪Surat Al-Hujuraat Aya ya 10.
➡Na kwa jinsi jambo hili lilivyochukiza hadi kwamba Allaah سبحانه وتعالى Anakataa kupokea amali za watu Waliogombana /waliokhasimiana mpaka wapatane, na hawasamehe watu hao⤵
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((تُعرض الأعمال في كل أثنين وخميس فيغفر الله لكل أمريء لايشرك بالله شيئاً، إلا إمرءاً بينه وبين أخيه شحناء فيقول: اتركوا هذين حتى يصطلحا)) رواه مسلم
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba kasema Mtume صلى الله عليه وسلم: Amali njema (vitendo vyema) hutandazwa kila Jumatatu na Alkhamiys, kisha Allaah Humghufuria kila mtu asiyemshiriki kitu Allaah, isipokuwa mtu aliyekuwa baina yake na baina ya ndugu yake uhasama, Husema: Waacheni hawa wawili mpaka wapatane))
↪Imepokelewa na Imaam Muslim
Kwa hiyo ni hatari kubwa kwa waliogombana na hawataki kusameheana watambue kuwa wanapoteza umri wao bure kutenda Mema na hali kumbe havipokelewi vitendo hivyo hadi wapatane. Kwahiyo ni Wajibu kusameheana kwanza ili utaraji Malipo kwa Allaah.
Njia za kupatanisha Waliogombana
1⃣Kwanza tia nia kuwa unafanya kupata Radhi na ujira mkubwa kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى, na muombe Allaah سبحانه وتعالى Akuwafikie jambo hili.
2⃣Msikilize kila mmoja malalamiko yake.
3⃣Ukishajua sababu ya ugomvi, watajie hatari ya kuhasimikiana kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم .
4⃣Tafuta wakati na sehemu munaasib kwa wote wawili.
5⃣Ikibidi kusema uongo, inafaa katika jambo hili kwa kutaka kumridhisha mmojawao ili kuleta suluhisho kama alivyoruhusu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika Hadiythi⤵
((لَيْسَ الْكَذابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خيرا أو يقول خيرا)) رواه البخاري ومسلم
((Si muongo yule anayesuluhusha watu kwa kusema uongo, kwani anaarifu mema au anasema mema [kwa lengo la kusuluhisha]))
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhariy na Muslim
6⃣Fanya uadilifu, usipendelee hata kama mmoja ni jamaa yako wa karibu au unampenda zaidi.
➡Amesema Allaah سبحانه وتعالى⤵
((...فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ))
((…basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Allaah Anawapenda wanaohukumu kwa haki))
↪Surat Al-Hujuraat Aya ya 9.
➡Na Anasema tena Allaah سبحانه وتعالى ⤵
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاء لِلّهِ وَلَوْ عَلَى أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْن وَالأَقْرَبِينَ إِِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقَيرًا فَاللّهُ أَوْلَى بِهِمَا فَلاَ تَتَّبِعُواْ الْهَوَى أَن تَعْدِلُواْ وَإِن تَلْوُواْ أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ))
((Enyi mlioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Allaah, ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Allaah anajua vyema mnayoyatenda))
↪Surat An-Nisaa Aya ya 135
7⃣Wakishapatana In shaa Allaah omba du'aa Allaah سبحانه وتعالى Awaendeleze masikilizano na mapenzi baina yao na muombe pia Akutakabalie juhudi yako.
Mwisho tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema.
Aamiyn.
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2USSrfb i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni