Translate

Jumapili, 28 Aprili 2019

Nani Anawajibika Kufunga?

                                                 Je,Ni nani Anawajibika Kufunga...?


Maulamaa wamekubaliana kufunga ni wajibu kwa mwenye akili timamu, Baleghe, mwenye afya na mkazi wa mji. Tukiongezea wanawake waliotwaharika na hedhi na nifasi.

Kwa wale ambao Swawm si wajibu juu yao ni wale ambao hawana akili timamu, hawajabaleghe.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
“Kalamu (kurekodiwa ‘amali) imeinuliwa (hairekodi) kwa watu watatu: anayepatwa na usingizi mpaka aamke, mtoto mpaka afike umri wa kubaleghe, na aliorukwa na akili mpaka atakapopata akili timamu.” [Hadiyth imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jami´, na. 3513 na Imerikodiwa na Abu Daawuwd].

Ama kwa wale wasioweza kufunga  ni kutokamana na maneno Yake Allaah:

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini (akafunga baadhi ya siku); basi (akamilishe) idadi (ya siku anazotakiwa kufunga) katika siku nyinginezo.” [Suwratul-Baqarah 02: 184].
Ikiwa mgonjwa au msafiri atafunga basi inawatosheleza, ama wakichukua ruhsa ya kula hapo wameondolewa uzito. Ama wakiamua kufunga kwa kuwa wanataka kufunga hapo pia wako sawa.

Ni kupi bora: Kutofunga au Kufunga?

Ikiwa mgonjwa au msafiri hawatoona tabu yoyote katika kufunga, basi kufunga kunapendekezwa. Ama wakikhofia kupata tabu kutokamana na kufunga, basi hapo kutofunga kunapendekezwa.
Abu Sa’iyd al-Khudriy ameelezea:
‘’Tulikuwa vitani na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) wakati wa Ramadhwaan. Wengine katika sisi walikuwa wamefunga na wengine walivunja Swawm zao. Wale waliofunga hawakuwaona waliovunja Swawm zao kuwa wako makosani na waliokula pia hawakuwaona waliofunga kuwa wako na makosa. Waliona wenye uwezo wa kufunga (walifunga) na hilo ni jambo zuri. Na ambao hawakuweza kufunga walivunja Swawm zao kwa udhaifu wa kufunga (hawakufunga) na hili pia ni jambo zuri.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan At-At-Tirmidhiy na. 574. Pia imerikodiwa na Imaam Muslim].

Ushahidi wa wanawake wasio Twahara kuwa hawafungi ni Hadiyth ya Abu Sa´iyd ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Je, si kwa kesi kwamba anapopatwa na damu yake ya mwezi, haswali wala hafungi? huo ni upungufu katika Dini yake.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy, katika Mukhtaswar Swahiyh Al-Al-Bukhaariy na. 951. Imerikodiwa na Imaam Al-Al-Bukhaariy].

Ikiwa mwanamke asiyo Twahara atafunga basi swawm yake haikubaliki kwani  katika masharti ya kukubalika swawm ya mwanamke ni awe katika Twahara. Mwanamke pia itamlazimu alipe siku alizokosa kufunga. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:
“Tulipokuwa tukipatwa na siku zetu za ada wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) tuliamrishwa kulipa Swawm za siku tuliokosa kufunga na hatukuamrishwa kulipa Swalah tulizokosa.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan At-Tirmidhiy na.630. Imerikodiwa na Imaam Muslim, Abu Dawuud, At-Tirmidhiy na An-An-Nasaaiy].

 Na   Allaah   anajua   zaidi



http://bit.ly/2IMYiB6 i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...