Translate

Ijumaa, 26 Aprili 2019

2. Mgonjwa asiyeweza kutawadha wala hana mtu wa kumsaidia kutia wudhuu´ ajitwaharishe vipi?

Swali 02: Siwezi kujitia wudhuu´ na sina mtu wa kunisaidia. Je, nifanye Tayammum pamoja na kuzingatia kwamba hospitali kila siku inasafisha kuta, ardhi na chini. Vipi nifanye Tayammum na hali ni kama hiyo uliyotaja?

Jibu: Mgonjwa akiwa hana ambaye atamtia wudhuu´ na wala hawezi kutawadha mwenyewe, basi afanye Tayammum. Amesema (Subhaanah):

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

“Mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akija kutoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Amepewa udhuru ambaye hawezi kuyatumia maji na kufanya Tayammum. Ni lazima kwake kuswali kwa wakati pasi na wudhuu´ wala Tayammum. Amesema (Subhaanah):

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yale niliyokukatazeni yaacheni na yale niliyokuamrisheni basi mcheni Allaah muwezavyo.”

Katika baadhi ya safari pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wako Maswahabah walioswali pasi na wudhuu´ wala Tayammum. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakemea kwa kitendo hicho. Hapo ilikuwa ni katika ile safari ambapo ´Aaishah alipoteza mkufu wake na baadhi ya Maswahabah wakaenda kumtafuta kwa amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini hata hivyo hawakumpata. Wakati wa swalah ukafika wakiwa hawana wudhuu´ na kipndi hicho Tayammum ilikuwa haijawekwa katika Shari´ah. Kisha Tayammum ikawekwa katika Shari´ah kwa sababu ya tukio hili. Hili ndilo la wajibu. Mgonjwa akiwa si muweza wa kutumia maji na hakuna mtu ambaye anaweza kumtawadhisha, basi lazima kwake kufanya Tayammum kwa kuwepo udongo msafi chini ya kitanda ndani ya chombo ambao atafanya Tayammum kwao na hilo litamtosha asihitajie wudhuu´. Haijuzu kufanya mchezo na jambo hili. Bali ni lazima kwa hospitali zote kutilia umuhimu jambo hili.

Ni lazima kwa mgonjwa kabla ya kutawadha na kabla ya kufanya Tayammum ajisafishe kinyesi au mkojo kwa kutumia maji au mawe. Si lazima iwe maji. Bali itamtosha kwake kujisafisha kwa kitambara kisafi na mfano wake kama vile mawe, udongo, mti na vyenginevyo. Muhimu uchafu uondoke. Ni lazima afute isiwe chini ya mara tatu. Pasiposafika kwa kufanya hivo basi azidishe mpaka kupatikane msafiko. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujisafisha kwa mwe afanye witiri.”

 Pia kutokana na yale yaliyothibiti kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikataza kujisafisha chini ya vijiwe vitatu na kwamba amekataza kujisafisha kwa mifupa na kinyesi. Havisafishi.”

[1] 05:06

[2] 64:16



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2L6ejny
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...