Translate

Jumapili, 28 Aprili 2019

Mambo Sita Yanayobatilisha Swawm

Mambo Sita Yanayobatilisha Swawm
                                                                                               
         
1. na 2. Kula au kunywa kwa kukusudia.

3. Kujitapisha kusudi.

4. na 5. Mwanamke atakapopata ada yake mwezi akiwa katika swawm.

6. Kitendo cha Jimai.


Mambo Yaliyopendekezwa kwa Mwenye Kufunga

Imependekezwa kwa mwenye kufunga afuate Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) katika kujitayarisha na swawm yake nayo ni haya yafuatayo;

1. Kula daku

Amehadithia Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) amesema:

‘’Kuleni daku, kwani kula huko daku kuna baraka.” [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Nasaa’y na Ibn Maajah].

Na ‘’kuleni daku’’ hata kama kwa kunywa maji inatosheleza. ´Abdullaah Ibn ´Amr amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Kuleni daku japo kwa kunwa tama la maji.’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2945 imeripotiwa na Ibn Hibbaan].

Pia Imependekezwa kuchelewesha kula daku. Amehadithiya Anas kutoka kwa Zayd ibn Thabit ambaye amesema:

‘’Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikula daku kisha akatoka kwenda kuswali. Anas akamuuliza “Kulikuwa na muda gani baina chakula cha daku na adhaana?” Akajibu: “Ilikuwa kiasi cha kusoma Aayah khamsini za Qur-aan".[Imeripotiwa na Imam Al-Bukhaariy na  Muslim].

Pia ameruhusiwa amalize chakula chake anaposikia Adhaana ya Fajr. Abu Hurayrah amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
“Endapo mmoja wenu atasikiya adhaana na mkononi mwake ana kinywaji, asirudishe kinywaji hicho mpaka aridhike nacho.’’[yaani anywe mpaka amalize haja yake].[Imesahihishwa na Shaykh al-Albaaniy katika al-Jami' as-Swaghiyr na.607].

2. Kujiepusha na maneno ya Upuuzi na mambo yasofaidisha Swawm yako.

Amehadithia Abu Hurayrah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Ikiwa mmoja wenu yuko ndani ya swawm ajiepushe na kitendo cha jimai na mabishano. Na kukitoka mmoja anataka kupigana nawe basi mwambiye ‘’Mimi Nimefunga’’.[Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy]. Tena amehadithiya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Yeyote ambaye hatowacha kusema uongo na kutenda kwa uongo basi Allaah (SubhanaHu wa Ta’ala) hana haja yake kwa kuwacha chakula chake na kinywaji chake’’.[Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika mukhtasar Swahiyh Al-Al-Bukhaariy na.921].

3. Kuwa na moyo kutoa na kujifunza Kusoma Qur-aan

Ibn ´Abbaas amesema: ’’Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikuwa mwenye moyo wa kutoa mali katika watu wote na akifanya vizuri kabisa. Alikuwa akitoa zaidi katika mwezi wa Ramadhwaan anapoonana na Malaika wa Allaah Jibriyl (´alayhis-Salaam). Jibriyl anaonana naye kila usiku wa Ramadhwaan mpaka mwezi umalizike. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) atasoma naye Qur-aan. Anapoonana na Jibriyl, alikuwa na moyo zaidi wa kufanya mema kuliko kuifadisha swawm yake’’. [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim].

4. Kukimbilia (kuharakisha) kufungua swawm

Sahl Ibn Sa'd amehadithiya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:
’’Watu watakuwa katika kheri endapo watakimbilia kufungua swawm zao’’.

5. Kufungua Swawm na yale yaliotajwa katika Hadiyth ikiwa ni rahisi kufanya hivo.

Anas amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikuwa akifunguwa swawm yake na Tende zilioiva kabla kusali. Kama si zilioiva alikuwa akifungua na Tende kavu. Kama hiyo pia haikupatikana basi alikuwa akifunguwa na kinywaji cha maji. [Ni Hadiyth Hasan Swahiyh katika al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2065]


Na  Allaah  anajua  zaidi


http://bit.ly/2IO3Afo i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...