Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) au Mwenye Kunyonyesha
Mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha ambaye hana uwezo wa kufunga ama ambaye anahofia afya ya mtoto wake anaweza asifunge, atalisha maskini mmoja na hawajibiki kuilipa siku aliyokula. Ibn ´Abbaas amesema:
“Ruhusa amepewa mtu mzima mume au mke ambapo wataoneleya tabu kufunga, hawatofunga ambapo hawatopendeleya kufunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ya kufunga. Kisha hawatalipa siku walizokosa kufunga hii iliondolewa baada ya Aayah hii:
وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ
“Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).” (Suuratul Baqarah 02 : 184)
Baada ya hapo ikahakikishwa kuwa mtu mzima mume au mke ambao hawawezi kufunga na mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha, ikiwa watahofia, hawatafunga na watalisha maskini kwa kila siku ambayo hawakufunga. [Msururu wa Riwaayah hii ni madhubuti imeripotiwa na Al-Bayhaqiy]. Pia imerikodiwa kuwa alisema, ikiwa wakati wa Ramadhwaan mwanamke mwenye mimba anahofia afya yake, au mwenye kunyonyesha anahofia afya ya mtoto wake, hawatafunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga na hawatalipa siku hizo kwa kufunga. [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.19].
Nafi’iy alisema ‘’Mmoja katika mabanati wa Ibn ´Umar aliolewa na mwanamume wa ki-Quraysh. Akapata mimba na wakati wa Ramadhwaan anashikwa na kiu sana. Ibn ´Umar akamwambiya funguwa swawm yako na ulishe masikini kwa kila siku.’’[Msururu wa Riwaayah ni Swahiyh na Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.20. Imerikodiwa na ad-Daraqutniy].
Kiwango gani cha chakula anawajibika kulisha?
Imeelezwa kwamba Anas Ibn Malik alidhoofika sana na hakuweza kufunga mwaka mzima akatayarisha sufuriya THARIYD (Mkate na nyama uliolowana katika supu) kisha akaalika masikini thelathini akawalisha mpaka wakaridhika’’. [Msururu wa Riwaayah hii ni Swahiyh pia imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl, mjallad 4 uk.21 imerikodiwa na ad-Daraqutniy].
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2IMDtFN i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni