Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Ndugu Muislamu, jitahidi utekeleze ‘ibaadah hii adhimu kwa wingi ya kusoma na kuhifadhi Qur-aan kwa sababu fadhila na thawabu zake ni nyingi na ‘adhimu mno kama tunavozinukuu baadhi yake humu.
Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza kuisoma) Qur-aan japo mara moja katika mwezi huu wa Ramadhwaan kwa sababu mwezi huu ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ
Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 184]
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾
121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake; hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika. [Al-Baqarah:121]
Imaam As-Sa’diy (Rahimahu-Allaah) amesema kuhusu Tafsiyr ya Aayah hiyo tukufu: “Allaah (Ta’aalaa) Anatujulisha kwamba wale ambao wamepewa Kitabu na Akawafanyia ihsaan kwa ujumla kwamba wao “Wanakisoma kwa haki ipasavyo kusomwa kwake” inamaanisha: Kuifuata kama ipasavyo kuifuata, na “tilaawah” (kuisoma) ina maana ni kuifuata yaani kuhalalisha Aliyoyahalalisha na wanaharamisha Aliyoyaharamisha, na wanafanyia kazi hukmu zake, na wanaamini Mutashaabihaat (Aayah zisizokukwa wazi maana yake), na hao ndio watu wenye furaha katika Ahlul-Kitaab, ambao hutambua neema za Allaah na wakazishukuru na wakamwamini kila Rasuli wala hawafarikishi baina yao, basi hao ndio Waumini wa kweli, si kama wale wanaosema: “Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu” na wanayakanusha yale yaliyokuja baada yake.” [Al-Baqarah: 91]
Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan
1. Kusoma Qur-aan Ni Kama Kufanya Biashara Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambayo Mtu Hapati Khasara.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾
Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea.
لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾
Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Faatwir: 29-30]
2. Aliye Bora Kabisa Ni Ambaye Anajifunza Na Kuifundisha Qur-aan
عن عثمانَ بن عفانَ رضي الله عنه أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلّم قالَ: ((خَيرُكُم مَنْ تعَلَّمَ القُرآنَ وعَلَّمَه)) صحيح البخاريِّ
Imepokelewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur-aan kisha akaifundisha)) [Al-Bukhaariy]
3. Anayeisoma Kwa Mashaka Hupata Thawabu Mara Mbili
عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ)) البخاري ومسلم
Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu watiifu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Imekusudiwa ni mtu mwenye ulimi mzito au ambaye ndio kwanza anaanza kujifunza na hupata shida kuisoma, lakini inampasa Muislamu ajitahidi kujifunza kuisoma kisawasawa ipasavyo.
4. Watu Wanaoshikamana Na Qur-aan Ni Watu Bora Kabisa Mbele Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ: ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ)) أحمد و إبن ماجه
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Anao watu wa aina mbili Anaowapenda kati ya watu)). Wakamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah ni nani hao? Akasema: ((Hao ni watu wa Qur-aan na ni watu wa Allaah, ni makhsusi Kwake [Awapendao]))[Ahmad, Ibn Maajah]
5. Mfano Wa Anayeisoma Qur-aan Ni Harufu Na Ladha Nzuri, Kinyume Na Asiyeisoma
عن أبي موسى الأشْعَريِّ رضي الله عنه أنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلّم قالَ ((مثلُ المؤمنِ الَّذِي يقرأ القرآنَ مَثَلُ الأتْرُجَّةِ ريحُها طيبٌ وطعمُها طيّبٌ، ومثَلُ المؤمِن الَّذِي لاَ يقرَأ القرآنَ كمثلِ التمرة لا ريحَ لها وطعمُها حلوٌ)) البخاري ومسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash'ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Mfano wa Muumini ambaye anayesoma Qur-aan ni kama tunda la Utrujjah; harufu yake nzuri na ladha yake nzuri. Na mfano wa Muumini asiyesoma Qur-aan mfano wake kama tende zisizokuwa na harufu lakini zina ladha tamu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Utrujjah ni tunda linalofanana na ndimu yenye rangi ya chungwa inayokaribia rangi ya dhahabu. Tunda hilo linajulikana kama tufaha la ki-Ajemi, lina harufu nzuri.
6. Anayeisoma Qur-aan Hupata Thawabu Kwa Kila Herufi Anayoitamka
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ الله عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللَّهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا لَا أَقُولُ الم حَرْفٌ وَلَكِنْ أَلِفٌ حَرْفٌ وَلَامٌ حَرْفٌ وَمِيمٌ حَرْفٌ))
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesoma herufi moja katika Kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja)) [At-Tirimidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2910), Swahiyh Al-Jaami'(6469), As-Silsilah Asw-Swahiyhah(3327)]
7. Anayeisoma Qur-aan Itakuwa Ni Shafaa’ah (Kiombezi) Siku Ya Qiyaamah
عن أبي أُمَامَةَ الْبَاهِلِي رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِه)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Someni Qur-aan kwani itakuja siku ya Qiyaamah kuwa ni Shafaa’ah kwa swahibu yake [mwenye kuisoma]) [Muslim]
8. Qur-aan Humnyanyua Mtu Daraja Ya Juu Na Humdhalilisha Asiyeandamana Nayo
قَالَ عُمَرُ: أَمَا إِنَّ نَبِيَّكُمْ قَدْ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الْكِتَابِ أَقْوَامًا، وَيَضَعُ بِهِ آخَرِينَ)) صحيح مسلم
‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Ama hakika Nabiy wenu amesema: ((Allaah Atawanyanyua baadhi ya watu kwa Kitabu hiki (Qur-aan) na Atawadhalilisha wengine kwa kitabu hiki)) [Muslim]
9. Mwenye Kuihifadhi Qur-aan Na Kuifanyia Kazi Atapandishwa Daraja Za Jannah
عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((يُقَالُ لِصَاحِبِ الْقُرْآنِ: اقْرَأْ وَارْتَقِ وَرَتِّلْ، كَمَا كُنْتَ تُرَتِّلُ فِي الدُّنْيَا، فَإِنَّ مَنْزِلَكَ عِنْدَ آخِرِ آيَةٍ تَقْرَؤُهَا)) رواهالترمذي (2914) وقال: هذا حديث حسن صحيح، وصححه الألباني في صحيح الترمذي
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Huambiwa Swahibu wa Qur-aan: “Soma na panda juu (daraja za Jannah) na uisome kwa Tartiyl (ipasavyo kwa hukmu za Tajwiyd) kama ulivyokuwa ukiisoma ulipokuwa duniani, kwani makazi yako ni pale utakapofika katika Aayah ya mwisho utakayoisoma”)). [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyhna ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy na Swahiyh Al-Jaami’]
Wengi kati ya ‘Ulamaa wamesema kuwa aliyekusudiwa kuwa ni “Swaahibul-Qur-aan” ni mwenye kuihifadhi na kuifanyia kazi wala si kuihifadhi bila ya kuifanyia kazi au kuisoma bila ya kuhifadhi.
Na Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah) amesema: “Tambua kwamba iliyokusudiwa kuhusu “Swahibu wa Qur-aan” ni mwenye kuihifadhi moyoni… [Silsilah Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (5/284)
Na amesema Ibn Hajar Al-Haytamiy (Rahimahu-Allaah): “Khabari iliyotajwa ni makhsusi kwa anayeihifadhi moyoni si kwa anayeisoma tu…” [Al-Haytamiy, uk. 113]
10. Wanaosoma Na Kujifunza Qur-aan Huteremka Malaika Kuwazunguka Kwa Utulivu Na Rahmah
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلَّا نَزَلَتْ عَلَيْهِمْ السَّكِينَةُ وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ وَحَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ وَذَكَرَهُمُ اللَّهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hawakusanyiki pamoja watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah, na wanafundishana baina yao, ila huwateremkia utulivu na hufunikwa na Rahmah na Malaika huwazunguka na Allaah Anawataja mbele ya [Malaika] aliokuwa nao))[Muslim Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad]
Pia:
عن أُسَيْدَ بْنَ حُضَيْرٍ بَيْنَمَا هُوَ لَيْلَةً يَقْرَأُ فِي مِرْبَدِه، إِذْ جَالَتْ فَرَسُهُ، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أُخْرَى، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا. قَالَ أُسَيْدٌ: "فَخَشِيتُ أَنْ تَطَأَ يَحْيَى فَقُمْتُ إِلَيْهَا فَإِذَا مِثْلُ الظُّلَّةِ فَوْقَ رَأْسِي فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". قَالَ: "فَغَدَوْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ بَيْنَمَا أَنَا الْبَارِحَةَ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ أَقْرَأُ فِي مِرْبَدِي إِذْ جَالَتْ فَرَسِي". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَانْصَرَفْتُ وَكَانَ يَحْيَى قَرِيبًا مِنْهَا خَشِيتُ أَنْ تَطَأَهُ, فَرَأَيْتُ مِثْلَ الظُّلَّةِ فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تِلْكَ الْمَلَائِكَةُ كَانَتْ تَسْتَمِعُ لَكَ وَلَوْ قَرَأْتَ لَأَصْبَحَتْ يَرَاهَا النَّاسُ مَا تَسْتَتِرُ مِنْهُمْ))
Imepokelewa kutoka kwa Usayd bin Khudhwayr, kwamba alipokuwa akisoma akiwa katika mirbad yake, farasi wake alishtuka. Akasoma, akashtuka tena, akasoma akashtuka tena. Akasema Usayd: Nikaogopa asije kumkanyaga Yahyaa (mwanawe). Nikainuka kumwendea (farasi) nikaona kitu kama kivuli juu ya kichwa changu kama kina kandili kikipanda mbinguni hadi kikapotea. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asubuhi yake nikamwambia: “Ee Rasuli wa Allaah, jana usiku nilipokuwa katika mirbad yangu nikisoma Qur-aan, farasi wangu alishtuka! Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr)). Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr)). Akasema niliondoka kwani Yahyaa alikuwa karibu naye, nikakhofu asimkanyage. Nikaona kama kivuli kikiwa na taa kinapanda juu hadi kikapotea. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hao ni Malaika walikuwa wakikusikiliza, lau ungeliendelea kusoma hadi asubuhi watu wangelikiona kisingelipotea)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
Mirbad – makazi ya mifugo ya farasi au ngamia.
11. Kuhifadhi Na Kujifunza Maana Ya Qur-aan Ni Bora Kuliko Mapambo Ya Dunia
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِي الصُّفَّةِ فَقَالَ: ((أَيُّكُمْ يُحِبُّ أَنْ يَغْدُوَ كُلَّ يَوْمٍ إِلَى بُطْحَانَ أَوْ إِلَى الْعَقِيقِ فَيَأْتِيَ مِنْهُ بِنَاقَتَيْنِ كَوْمَاوَيْنِ فِي غَيْرِ إِثْمٍ وَلَا قَطْعِ رَحِمٍ؟)) فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ نُحِبُّ ذَلِكَ قَالَ: ((أَفَلَا يَغْدُو أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَسْجِدِ فَيَعْلَمُ أَوْ يَقْرَأُ آيَتَيْنِ مِنْ كِتَابِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ خَيْرٌ لَهُ مِنْ نَاقَتَيْنِ وَثَلَاثٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ ثَلَاثٍ وَأَرْبَعٌ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَرْبَعٍ وَمِنْ أَعْدَادِهِنَّ مِنْ الْإِبِلِ))
Imepokelewa toka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu)ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia wakati tulikuwa katikaSwuffah akauliza: ((Kuna yeyote miongoni mwenu anayetaka kwenda soko la Butw-haan au [soko] la Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili wakubwa na walionona bila ya kutenda dhambi au kukata undugu?)) Tukajibu kwamba sote tunapenda kufanya na kupata hivyo. Kisha akasema: ((Basi aende mmoja wenu Masjid akajifunze au asome Aayah mbili katika Kitabu cha Allaah (‘Azza wa Jalla), pindi akifanya hivyo, basi ni bora kuliko ngamia wawili. Na Aayah tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa ngamia))[Muslim, Abuu Daawuwd, Ahmad]
Swuffah: Sehemu katika Masjid Ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) waliyokuwa wakikaa Maswahaba ambao hali zao walikuwa ni masikini.
Butw-haan: Bonde lilioko kusini mwa mji wa Madiynah kuelekea upande wa Magharibi karibu na Jabali la Sal’. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitawadha katika bonde hilo siku ya vita vya Khandaq
Al-'Aqiyq: Bonde maarufu kabisa katika mjia wa Madiynah au eneo la Al-Hijaaz yote. Liko umbali wa maili kilometa mia Kusini na linaelekea upande wa Mashariki. Linajulikana kuwa ni ‘Bonde lilibarikiwa’.
12. Mwenye Kuhifadhi Qur-aan Huvalishwa Taji Siku Ya Qiyaamah
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَجِيءُ الْقُرْآنُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ: يَا رَبِّ حَلِّهِ، فَيُلْبَسُ تَاجَ الْكَرَامَةِ،ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ زِدْهُ، فَيُلْبَسُ حُلَّةَ الْكَرَامَةِ، ثُمَّ يَقُولُ: يَا رَبِّ ارْضَ عَنْهُ،فَيَرْضَى عَنْهُ فَيُقَالُ لَهُ: اقْرَأْ وَارْقَ، وَتُزَادُ بِكُلِّ آيَةٍ حَسَنَةً))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Qur-aan itakuja siku ya Qiyaamah na itasema: “Ee Rabb, Mpambe” [Mwenye kuhifadhi Qur-aan]. Kisha atavalishwa taji la takrima. Kisha [Qur-aan] itasema: “Ee Rabb muongeze”. Kisha huyo mtu atavishwa nguo ya takrima. Kisha itasema: “Ee Rabb Ridhika naye”. Allaah, Ataridhika naye. Kisha ataambiwa: “Soma na panda”. Atapokea thawabu zaidi ya mema kwa kila Aayah [atakayosoma])) [At-Tirmidhy na Al-Haakim, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2915),Swahiyh At-Targhiyb (1425), Swahiyh Al-Jaami’ (8030)]
13. Mwenye Hifdh Na ‘Ilmu Ya Qur-aan Huwa Na Nuru Kaburini Na Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Atakuwa Shahidi Wake Siku Ya Qiyaamah
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضى الله عنهما قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَجْمَعُ بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ مِنْ قَتْلَى أُحُدٍ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ ثُمَّ يَقُولُ : ((أَيُّهُمْ أَكْثَرُ أَخْذًا لِلْقُرْآنِ)) فَإِذَا أُشِيرَ لَهُ إِلَى أَحَدِهِمَا قَدَّمَهُ فِي اللَّحْدِ، وَقَالَ: ((أَنَا شَهِيدٌ عَلَى هَؤُلاَءِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ)). وَأَمَرَ بِدَفْنِهِمْ فِي دِمَائِهِمْ، وَلَمْ يُغَسَّلُوا وَلَمْ يُصَلَّ عَلَيْهِمْ.البخاري
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwakusanya watu wawili waliokufa katika vita vya Uhud katika nguo moja kisha aliuliza: ((Nani katika hao mwenye Qur-aan zaidi?)) Anapojulishwa mmoja kati ya hao, humtanguliza kaburini, na akasema: ((Mimi ni Shahidi wa hawa Siku ya Qiyaamah)) [Al-Bukhaariy]
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2INr2cE i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni