Mwezi wa Ramadhwaan unathibitishwa kuonekana kwake na mtu mmoja mwenye kujulikana kwa ukweli na kumcha kwake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) au kwa kutimiza siku thelathini za mwezi wa Sha’abaan.
Ibn ´Umar amesema watu walikuwa wakitafuta kuandama kwa mwezi. nikamjulisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) kuwa mimi nimeuona mwezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akafunga na akaamrisha watu wafunge.” [Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab I’rwa al-Ghaliyl na. 908 na Imeripotiwa na Abu Daawuwd].
Ikiwa mwezi haukuandama, kwa sababu ya kufunikwa na mawingu au kwa sababu nyingine basi hapo mwezi wa Sha’abaan utatimizwa kwa siku thelathini kama alivyoripoti Abu Hurayrah katika Hadiyth iliyo hapo juu.
Lakini mwezi wa Shawwaal unatangazwa kuonekana kwa mashahidi wawili.’ ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Al-Khattwaab amesema: “Nilipokuwa nikikhutubia siku ambayo ni ya shaka (kama mwezi wa Ramadhwaan kama umekwisha ama la), nikasema: “Nilikaa na Maswahaba zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) nikawauliza wao. Wakaniambia mimi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alisema:
‘’Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi na tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake. Ikiwa kuna mawingu basi timizeni siku thelathini. Na Ikiwa Waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuonekana kwa mwezi basi fungeni na mfungue kwa kushuhudia kwao mwezi.’’ [Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab cha Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh al-Jamiy’ Asw-Swaghiyr na. 3811. Pia Imeripotiwa na Imaam Ahmad na An-Nasaaiy bila kipande kinachosema ‘’Waislamu wawili.’’].
Mtawala wa Makkah, Al-Haarith bin Hatwiyb amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alituambia sisi tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake munapouona mwezi. Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini mashahidi wawili wa kuaminika wakishuhudia kwa kuona mwezi tunatekeleza ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’ [Hadiyth Swahiyh angalia Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh Sunan Abiy-Daawuwd, na. 205. Imeripotiwa na Abu Daawuwd].
Tukiangalia ripoti mbili hizi,
’’Ikiwa waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuona mwezi, basi fungeni na fungueni’’katika Hadiyth ya Abdur-Rahmaan bin Zayd na:
‘’Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini watu wawili wenye kujulikana kwa ukweli wakasema wameuona mwezi tunatimiza haki za ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’ katika Hadiyth ya Al-Haarith wanaonyesha kwa kutilia mkazo, kuwa haifai kuanza kufunga au kumaliza kufunga kutokamana na ushahidi wa mtu mmoja pekee. Juu ya hilo, tangu kuanza kwa kufunga imeondolewa uzito kutokana na ushahidi (uliotolewa hapo juu), inawacha suala la kumaliza kufunga, ambalo halina ushahidi kwamba linatoshelezwa kwa ushahidi wa mtu mmoja pekee. Huu ni ufupi wa mjadala unaopatikana katika Kitabu ‘Tuhfah Al-Ahwadhiy’ [Mjalada wa 3, uk. 373-3749].
Tanbihi Ikiwa mtu atauona mwezi yeye peke yake, hafungi mpaka watu wafunge na hamalizi kufunga mpaka watu wamalize kufunga kama ilivyoripotiwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu), kwamba amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam):
‘’Swawm (kufunga) ni siku ambayo watu wanafunga. Na kumaliza kufunga ni siku ambayo watu wanamaliza kufunga. Na kuchinja ni katika siku ambayo watu wanachinja.’’ [Hadiyth Swahiyh. Angalia Swahiyh Al-Jami’ Asw-Swaghiyr, na. 3869]. Imehifadhiwa na Imaam At-At-Tirmidhiy ambaye amesema: ‘’Baadhi ya Maulamaa wanaifasiri Hadiyth hii kwa maana: “Kuanza kufunga na kumaliza kufunga kunatekelezwa na watu wote kwa pamoja na wakati mmoja.”
http://bit.ly/2J1hBWE i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni