Kutekeleza ´Ibaadah ya Kufunga Mwezi wa Ramadhwaan
Kufunga mwezi wa Ramadhwaan ni moja katika nguzo za Dini yetu ya Kiislamu na moja katika mambo ya lazima yampasayo kila Muislamu. Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Swawm kama ilivyoandikwa kwa wale ambao wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa.” [Suwratul Baqarah 02: 183].
Baada ya Aayah hii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema tena:
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
“Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe Hudan (Uongofu) kwa watu na hoja bayana za Al-Hudaa (Uongofu) na Al-Furqaan (Upambanuzi). Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi (atimize) idadi katika siku nyinginezo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; ili mkamilishe idadi na ili mumkabbiri Allaah (mseme: Allaahu Akbar) kwa kukuhidini na mpate kushukuru..” [Suwratul Baqarah 02: 185].
Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhuma) alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:
“Uislamu umejengewa katika (nguzo) tano: Kuthibitisha kidhati kuwa hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa Haqq ila Allaah, na kuthibitisha kidhati kuwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) ni Mtume Wake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kutekeleza ´Ibaadah ya Hajj kwa mwenye uwezo, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhwaan.”[Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim].
Waislamu wote wamekubaliana kuwa kufunga mwezi wa Ramadhwaan ni wajibu wa kila Muislamu na kuwa ni moja katika (nguzo) za Uislamu na ni jambo lenye kujulikana katika Dini yetu kwa kutekelezwa kwake. Yeyote atakayekanusha ´Ibaadah hii ya Kufunga mwezi wa Ramadhwaan kuwa si wajibu kwa kila Muislamu atakuwa amekufuru Kufru ambayo inamtoa katika Uislam.
Uzuri Wa Kutekeleza ´Ibaadah Ya Kufunga Mwezi Wa Ramadhwaan
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:
“Yeyote atakayefunga mwezi wa Ramadhwaan kwa Imani na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah basi Allaah Atamsamehe madhambi yake yote yaliyopita.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah].
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema tena, alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:
“Allaah amesema: “Kila ‘Amali ya mwanaadam ni yake yeye mja Wangu ila Swawm. Ni yangu Mimi na mimi ndiye Nitakayemlipa mja Wangu.”
Swawm ni kinga. Itakapofikia siku mmoja wenu amefunga ajiepushe na kufanya kitendo cha jimai na mabishano na watu. Na yeyote atakayetaka kupigana naye basi amwambie “Mimi nimefunga.” Naapa kwa jina la Allaah, Harufu inayotoka katika mdomo wa mwenye kufunga ni nzuri kwa Allaah kuliko harufu ya Misk. Kwa Mwenye kufunga ana furaha mbili: Furaha anapofungua Swawm yake na furaha pale atakapoonana na Mola Ameridhika kwa kufunga kwake.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy]
Sahl ibn S’ad (Radhiya Allaahu ´anhu) alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:
‘’Peponi kuna mlango unaitwa Ar-Rayyaan. Wale wenye kufunga wataingia peponi kupitia lango huu siku ya Qiyaamah na hakuna mwengine atakayepita katika mlango huu ila (wafungaji). Itaambiwa: ‘’Wako wapi waliokuwa wakifunga?” Watasimama na watapita katika mlango huu na watakapomalizika kuingia wote (wafungaji) utafungwa na hakuna mwengine atakayepita hapo tena.“[Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, At-At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na An-Nasaaiy].
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2IMOG98 i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni