Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa mwanamke kuhudhuria swalah ya ijumaa?
Jibu: Mwanamke kuhudhuria ijumaa na swalah za mkusanyiko ni jambo ambalo halikuwekwa katika Shari´ah. Lakini hata hivyo linafaa. Dalili ya hili ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:
“Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokamana na misikiti ya Allaah na nyumba zao ni bora kwao.”
Bora kwa mwanamke ni yeye kuswali nyumbani kwake. Ni mamoja swalah ya ijumaa na swalah ya mkusanyiko. Lakini akihudhuria hatumkatazi midhali atakuja msikitini hali ya kuwa si mwenye kuonyesha mapambo wala mwenye kujipulizia manukato yenye kutoa harufu inayoweza kunuswa na yule aliye pembezoni mwake.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2GB8lFD
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni