Swali 16: Ni ipi hukumu ya mwenye kula au kunywa mchana wa Ramadhaan kwa kusahau?
Jibu: Hakuna neno juu yake na swawm yake ni sahihi. Allaah ((Subhaanah) amesema mwishoni mwa Suurah “al-Baqarah”:
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]
Imesihi kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwamba Allaah (Subhaanah) amesema:
“Nimefanya hivo.”
Pia imethibiti kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kusahau ambapo akala au akanywa basi aikamilishe swawm yake. Kwani si vyengine Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
[1] 02:286
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2GFXeww
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni