Translate

Jumatano, 24 Aprili 2019

15. Swawm ya Ramadhaan na kwenda kwa daktari wa meno

Swali 15: Mtu akipatwa na maumivu katika meno yake ambapo akaenda kwa daktari akamsafisha meno, akamtengeneza au akamg´oa jino lake – je, mambo hayo yanaiathiri swawm yake? Iwapo daktari atamdunga sindano ya kumpoza meno yake kuna athari yoyote juu ya swawm yake?

Jibu: Hayo yaliyotajwa hayana athari katika kusihi kwa swawm yake. Ni mambo yenye kusamehewa. Ajichunge asije kumeza dawa wala damu yoyote. Sindano hii iliotajwa haina athari yoyote juu ya kusihi kwa swawm yake kwa sababu haina maana ya kula wala kunywa. Kimsingi ni kwamba swawm ni yenye kusihi na kusalimika.



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2W35nAp
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...