Translate

Jumatano, 20 Februari 2019

Sifa za mja zimekadiriwa

´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kila kitu ni kwa Qadar, mpaka kushindwa na werevu.”[1]

Qadar hii imekusanya hali zote za mja, matendo yake na sifa zake, mpaka kushindwa na werevu. Hizi ni sifa mbili zilizo kinyume. Siku ya kwanza, ambayo ni kushindwa, inapelekea katika kutokuweza na ukhasirikaji. Sifa ya pili, ambayo ni werevu, ambao unapelekea kuwa na bidii katika kumtii Allaah.

Ushindwaji unaokusudiwa hapa ni ule wenye kusemwa vibaya ambao una maana yake ni kule mtu kutokuwa na matakwa. Kwa msemo mwingine uzembe. Haihusiani na ushindwaji wa kutokuwa na uwezo. Hii ndio maana ya Hadiyth ya ile Hadiyth nyingine inayosema:

“Tendeni! Kila mmoja amewepesishiwa kwa lile aliloumbiwa. Kuhusu wale wenye furaha wamerahisishiwa kutenda matendo yenye furaha na wale wasiokuwa na furaha wamerahisishiwa kutenda matendo yasiyokuwa na furaha.”[2]

Kuhusu wale wenye furaha wamerahisishiwa kutenda matendo yenye kuwafanya wakawa na furaha. Hayo ni kutokana na werevu wao, mafanikio yao na upole wa Allaah juu yao.

[1] Muslim (2655), Ahmad (5859) na Maalik (1663).

[2] al-Bukhaariy (4949) na Muslim (2647).



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2IpUXsf
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...