Swali
assalaamu alaykum je, nini hukumu ya kuwakilishana katika kuoa, yaani kuoa kwa niaba ya ndugu yako; ikiwa inafaa, je ni zipi taratibu zake?
Jibu
Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh
✅Naam, Kukiwa na dharura ya kukosekana kwako kwenye kufunga ndoa, unaweza kutoa idhini yako ima kwa maandishi au kwa njia ya simu inayothibitisha ni wewe na Walii (baba wa mke au babu au kaka) akawepo na mashahidi wawili na mahari.
✅Kwahiyo Ndoa Itajuzu kukipatikana hili
✅Na pia tambua kuwa lazima awepo Walii wa mwanamke unayetaka kumuoa, kukosekana Walii kunaifanya ndoa isiwe sahihi; yaani batili.
➡Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba⤵
*“Hakuna ndoa bila Walii.”*
↪Imepokelewa na Imaam Ibn Maajah, At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd na Al-Albaaniy kasema ni sahihi.
✅Lakini, ni bora zaidi kusubiri mwenyewe upatapo hiyo nafasi ya kwenda kufunga ndoa mwenyewe kwa sababu nyingi muhimu na zenye faida kwako wewe mwenyewe kuliko kumwakilisha mtu.
✅Kuwepo kwako(Yaani bwana Harusi) utapata Sunnah nyingi za jambo hilo, kuanzia kufungishwa ndoa na kuitikia mwenyewe kukubali kwako kumuoa huyo mke, vilevile utapata kufurahi na pia kuwa na wasaa wa kuwa na mkeo na kufanya yale ambayo mume na mke wanayafanya ya starehe na furaha, na mengine mengi katika siku hiyo adhimu ya furaha.
Na Allaah anajua zaidi
http://bit.ly/2IcWMst i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni