*Swali*
Assalam alaykum warahmatullah
Ndugu yangu nisaidie hapa yupo mtu mie namdai pesa zangu sasa juzi nnamkumbusha asema wacha nifanye process nichukue mkopo bank kisha nikupe pesa zako sasa akichukua huko bank kisha akanipa itakuwa sahih mm kutumia hizo pesa?
*Jibu*
Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh
✅Naam, Inajuzu Muislamu kuchukua Mkopo Bank kwa ajili ya Kulipa (Kufidia) Deni analodaiwa kwa Sharti tu Mkopo huo anaochukua Bank usiwe na *Riba*.
➡Ama ikiwa kuna Riba ndani yake basi Haijuzu na ni Haraam.
➡Hakika ni kuwa Allaah Aliyetukuka Ameharamisha kuchukua na kutoa ribaa katika njia zake zote.
➡Allaah (Subhaana wa Taala) Anasema: “Allaah Amehalalisha biashara na kuiharamisha ribaa”
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 275.
➡Na amesema tena Allaah(Subhaana wa Taala); “Enyi Mlioamini! Mcheni Allaah, na acheni yaliyobakia katika ribaa, ikiwa mmeamini. Na kama hamtafanya hivyo, basi fahamuni mtakuwa mmetanganza vita na Allaah na Mtume Wake”
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 278 – 279.3
➡Na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia kuwa: “Allaah Amemlaani mwenye kula ribaa, mwenye kuitoa na mashahidi wake na mwandishi wake”
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.
➡Na amesema tena Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu uovu wa ribaa: “Dirhamu ya ribaa anayokula mtu na huku anajua ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara thelathini na sita”
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad.
➡Amesema tena: “ribaa ina milango 73 iliyo nyepesi na sahali ni mtu kumuoa (kumuingilia) mamake”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Haakim.
Na Allaah anajua zaidi
Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*
https://ift.tt/2V83wct i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni