Swali 15: Baadhi wanafikiri kuwa ni wanachuoni tu ndio wanatakiwa kulingania katika dini ya Allaah na wengine hawahitajii kulingania kutokana na yale waliyojifunza. Unasemaje juu ya hilo?
Jibu: Sio ufikiriaji. Huu ndio uhakika wa mambo. Wanachuoni tu ndio wanatakiwa kulingania. Hata na mimi ninasema hivo. Hata hivyo kuna mambo ya wazi yanayojulikana na watu wote. Kila mtu aamrishe mema na kukataza maovu kwa kiasi na elimu yake. Aiamrishe familia yake Swalah na mambo mengine yaliyo wazi. Hili ni wajibu hata kwa wasiokuwa wasomi. Wanatakiwa kuwaamrisha wana wao kuswali Msikitini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Waamrisheni watoto zenu kuswali pindi wana miaka saba na wapigeni kwayo pindi wana miaka kumi na muwatenganisha kwenye vitanda.”[1]
“Nyote ni wachungaji na kila mmoja ataulizwa kwa kile alichokichunga.”[2]
Hili linaitwa uchungaji. Linaitwa kuamrisha mema na kukataza maovu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote yule mwenye kuona maovu, basi ayabadilishe kwa mkono wake. Ikiwa hawezi, ayabadilishe kwa mdomo wake. Ikiwa hawezi, ayabadilishe kwa moyo wake – hiyo ni imani dhaifu.”[3]
Asiyekuwa msomi anapaswa kuiamrisha familia yake na wengine kuswali, kutoa zakaah, kumtii Allaah na kujiepusha na maasi. Aidha aisafishe nyumba yake na madhambi na awalee watoto zake kwa uchaji Allaah. Hili linampasa hata kama si msomi. Kwa sababu linajulikana na kila mtu; hili ni jambo liko wazi.
Ama kuhusu fataawaa, halali na haramu, shirki na Tawhiyd, wanachuoni tu ndio wanasimamia hayo.
[1] Abu Daawuud (495). Hadiyth ni Swahiyh. Tazama ”Nasb-ur-Raayah” (1/298) kwa muundo kama huo.
[2] al-Bukhaariy (853).
[3] Muslim (49).
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2SHOdty
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni