08. Kufufuliwa kwa watoto
Miongoni mwa misingi ya imani yenye kumuokoa mtu na kufuru ni kuamini:
1- Kufufuliwa.
2- Malipo.
3- Hesabu.
4- Pepo.
5- Moto.
Yote haya ni haki. Allaah (Ta´ala) amesema:
"Kutoka humo [ardhini] Tumekuumbeni na katika hiyo [ardhi] Tutakurudisheni na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine.''20:55
"Na ukistaajabu basi cha ajabu ni maneno yao: “Je, sisi tukiwa mchanga, hivi kweli [tutafufuliwa] katika umbo jipya?” Hao ni wale waliomkanusha Mola wao. Hao watafungwa minyororo katika shingo zao. Na hao ndio watu wa Motoni, wao humo ni wenye kudumu."13:05
Katika Aayah kuna dalili yenye kuonesha kuwa yule mwenye kupinga juu ya kufufuliwa amekufuru na kwamba atadumishwa Motoni milele. Allaah atukinge na kufuru na matendo ya kikafiri.
09. Da´wah ya Mtume kwa watoto
Aayah hizi zinafahamisha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumwa ili awaamrishe watu kumuabudu Allaah peke yake na kuwakataza kumuabudu mwengine asiyekuwa Allaah.
Hii ndio dini yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo aliwalingania watu kwayo na akawapiga vita kwayo.
Allaah (Ta´ala) amesema:
"Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah na Dini yote iwe kwa ajili ya Allaah."08:39
Fitnah ni shirki.
Allaah (Ta´ala) alimtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa na miaka arubaini.
Miaka kumi aliwalingania watu katika kumuabudu Allaah peke yake na kuacha kumuabudu mwengine asiyekuwa Allaah.
Baada ya hapo akasafirishwa kupandishwa mbinguni.
Huko juu akafaradhishiwa kuswali swalah tano. Pindi Allaah (Ta´ala) alipomfaradhishia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hapakuwepo mkati kati yeyote baina yake na Allaah.
Baada ya hapo akaamrishwa kuhajiri. Akahajiri kwenda al-Madiynah. Vilevile akaamrishwa kutoka kwenda katika Jihaad.
Karibu miaka kumi akatoka kwenda kupigana Jihaad kwa ajili ya Allaah mpaka watu wakasilimu kuingia katika dini ya Allaah makundi kwa makundi. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofikisha miaka sitini na tatu na Allaah (Ta´ala) akaikamilisha dini kupitia kwake na akamfanya kufikisha ujumbe wa Allaah, ndipo akafariki. Swalah na salaam ziwe juu yake.
10. Mitume kwa watoto
Mtume wa kwanza ni Nuuh (´alayhis-Salaam) na Mtume wa mwisho ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Allaah (Ta´ala) amesema:
"Hakika Tumekufunulia Wahy kama Tulivyomfunulia Wahy Nuuh na Manabii baada yake."04:163
Allaah (Ta´ala) amesema tena:
"Na Muhammad si yeyote isipokuwa ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume."03:144
"Hakuwa Muhammad baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima kwa kila kitu ni Mjuzi."33:40
Mtume bora ni Nabii wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Watu bora baada ya Manabii ni Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh), halafu ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh), kisha ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na halafu ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Allaah awawie radhi wote.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: "Karne bora ni ya kwangu, kisha itayofuatia kisha itayofuatia." Al-Bukhaariy (2652) na Muslim (6635)
Vilevile ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atateremka kutoka mbinguni na atamuua ad-Dajjaal'' Muslim (7560).
NA ALLAAH ANAJUA ZAIDI
MWISHO MWISHO MWISHO
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2RdW0LU
via IFTTT
Translate
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
SWALI: Assalaam alaykum Naomba maana ya majina yeyote tuwapao watoto wetu AU mnielekeze wapi naweza kupata labda katika kitabu cha fas...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni