Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
✅Naam, Ndugu zangu katika Imaani, Swalah ina vigawanyo viwili tu ambavyo ni Swalah za faradhi na Swalah za Sunnah
1.Swalah Za Faradhi
✅Ni zile ambazo mwenye kuziacha kwa kusudi, Basi unakuwa unamuasi Allaah (Subhaana wa Taala).
➡Na Swalah hizi za Faradh ziko aina mbili ambazo ni⤵
(a) Fardhu ‘Ayn
➡Nazo ni zile ambazo ni lazima kwa kila aliyebaleghe na mwenye akili, mwanamke au mwanamume, aliye huru na mtumwa.
✅Hizi ni kama Swalah tano.
(b) Fardhu Kifaayah
➡Ni zile ambazo baadhi ya watu wakiziswali, basi haiwapasi wengineo.
✅Ni kama Swalah ya maiti.
2.Swalah Za Sunnah
✅Ni zile ambazo mwenye kuacha kuziswali kwa kusudi,basi unakuwa hamuasi Allaah (Subhaana wa Taala) .
➡Ni kama Sunnah zilizozoeleka na nyinginezo zitakazoelezewa katika milango ijayo.
✅Lakini imesuniwa kuziswali Swalah za Sunnah, na kuziacha ni makruhu.
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2HVnbeg
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni