✅Nguzo za Swalah maana yake ni zile ambazo ukiswali na ukaziacha kwa makusudi Swalah yako inabatilika, na ikiwa umeacha kwa kusahau, Swalah yako pia itakuwa haikukamilika hadi urejee kitendo chenyewe au urejee rakaa na kisha mwishoni utoe Sajdatus-Sahw.
➡Lakini ukiwa umesahau nguzo ya Takbiyratul-Ihraam, basi itakubidi uiswali Swalah upya tokea mwanzo.
Idadi ya Nguzo za Swalah ni 14 ambazo ni kama zifuatazo⤵
1.Kusimama katika Swalah za Fardh kwa yule mwenye uwezo.
➡Hapa Wanachuoni wengine wamesema nguzo ya kwanza ni Niyah kabla ya Kusimama lakini Niyah hii haitamkwi bali kitendo cha wewe kwenda kuswali unakuwa tayari ukeweka Niyah .
➡Allaah(Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema⤵
"Na simameni kwa ajili ya Allaah hali ya kuwa watiifu"
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 238.
➡Na Mtume Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swali hali ya kuwa umesimama, usipoweza, basi kwa kukaa na usipoweza basi kwa kulala ubavu"
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.
2.Takbiyrah ya kuhirimia (Takbiyratul-Ihraam) kwa tamko la Allaahu Akbar
➡Mtume Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ufunguo wa Swalah ni kujitwaharisha, na kuifunga ni Takbiyrah, na kuifungua ni kutoa Salaam"
↪Imepokelewa na Imaam Abu Daawuud na At-Tirmidhiy.
3.Kusoma Suratul-Faatihah katika kila rakaa.
➡Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: "Hapana Swalah kwa ambaye hakusoma Suratul Faatihah"
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy.
4.Kurukuu
5.Utulivu (Twumaaniynah) katika Rukuu.
6.I'itidaal (Yaani hapa inaingia na kunyanyuka kutoka katika Rukuu hadi anaponyooka mtu).
7.Utulivu katika I'Itidaal.
8.Kusujudu.
9.Utulivu katika kusujudu. Kutulia wakati wa kurukuu, kusujudu, kusimama, kukaa baina ya Sijdah mbili .
➡Mtume Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Kisha rukuu mpaka utulizane hali ya kurukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane sawa hali ya kusimama, kisha sujudu mpaka utulizane na hali umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane hali ya kuwa umekaa"
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy.
10.Kikao baina ya Sijdah mbili.
11.Utulivu katika kikao baina ya Sijdah mbili.
12.Tashahhud ya mwisho.
13.Kikao katika Tashahhud ya mwisho.
14.Salaam (Kutoa Salaam) ya kwanza.
Utahakikisha unafuatanisha yote hayo kama utaratibu ulivyopangika.
NA ALLAAH ANAJUA ZAIDI
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2GesxPW
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni