Translate

Ijumaa, 28 Desemba 2018

Mafunzo ya Swalah - Kusujudu

                                            MAFUNZO  YA   SWALAH  -  KUSUJUDU



Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh


Mswaliji anapoktaka kusujudu basi asujudu na wakati huo huo aseme "Allaahu Akbar" na huku atangulize magoti kabla ya mikono yake - iwapo kutakuwa urahisi wa kufanya hivo - la sivyo atangulize mikono yake kabla ya magoti yake.

Vidole vya miguu na mikono yake vinatakiwa kuelekea Qiblah .

Pia mswaliji anatakiwa kusujudu juu ya viungo vyake saba: paji la uso, pua, mikono yake miwili, magoti yake mawili na matumbo ya vidole vya miguu yake. Halafu aseme:

"Subhaana Rabbiy´ al-A´laa" 

"Utakasifu ni wa Mola, Aliye juu."


Mswaliji anatakiwa akariri hivo mara tatu au zaidi. Lakini kauli kuu waliyokubaliana maulamaa ni mara tatu.

Imependekezwa kuongezea juu yake:

"Subhaanaka, Allaahumma Rabbanaa wa bihamdik. Allaahumma Ighfir liy." 

"Ee Mola! Utakasifu na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe." al-Bukhaariy (761), Muslim (484), an-Nasaa´iy (1122), Abu Daawuud (877), Ibn Maajah (889) na Ahmad (06/43).


Vilevile aombe du´aa kwa wingi.

Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: "Katika Rukuu´ muadhimisheni Mola. Ama katika Sujuud jitahidini katika kuomba du´aa, kwani kuna matarajio mkaitikiwa"  Muslim (738), Abu Daawuud (742), Ahmad (1260) na (1801).

Mswaliji ajiombee kwa Mola Wake yeye du´aa na awaombee vilevile waislamu wengine mema ya duniani na ya Aakhirah. Afanye hivi sawa katika swalah ya faradhi na ya Sunnah.

Mswaliji anatakiwa vilevile kutanua mikono yake mbali na mbavu zake, tumbo mbali na mapaja yake, mapaja mbali na miguu yake na asiinamishe mikono yake juu ya ardhi.

Mtume  Muhammas(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Nyookeni katika Sujuud na wala mmoja wenu asiinamishe mikono yake kama inavyofanya mbwa."  al-Bukhaariy (779), Muslim (762) na an-Nasaa´iy (1098).



Na  Allaah  anajua  zaidi

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2GKfp6m
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...