Translate

Jumamosi, 29 Desemba 2018

HISTORIA FUPI YA TAASISI

The Islamic Foundation ni taasisi ya kidini yenye makao yake makuu manispaa ya Morogoro. Taasisi ilianzishwa mnamo mwaka 1996 na kusajiliwa rasmi tarehe 10/9/1998 wakati huo ikiwa inaitwa Morogoro Islamic Foundation ikiwa na idara kuu tatu tu, yaani Idara ya ujenzi, Idara ya Da’awa na Idara ya Yatima. Baada ya kuona waislamu wanaomba tufungue matawi mikoani ndipo bodi ya wadhamini ikaamua kubadilisha jina na kuitwa The Islamic Foundation. Kadri siku zilivyozidi kwenda taasisi ilizidi kukua kwa kutanua wigo wake na mwaka huohuo 1998 ilianzisha Idara ya Elimu kwa lengo la kusaidia kizazi cha kiislamu kwa kuwaandalia mazingira bora ya kupata elimu yao itakayowafaa hapa Duniani na kesho Akhera.

Kutokana na umuhimu wa vyombo vya habari kwa waislamu The Islamic Foundation iliamua kuanzisha idara ya habari mnamo mwaka 2002, tulipeleka maombi ya kufungua Redio na mnamo 2003 tuliruhusiwa kuanza kurusha matangazo ya Redio Imaan ambayo ilianzia kurusha matangazo Morogoro na baadaye kusambaa nchi nzima. Mwaka 2012 tuliona kuna tija ya kuanzisha Televisheni Imaan, hivyo The Islamic Foundation ilianza mchakato na kufanikiwa kuanzisha televisheni pekee ya kiislamu nchini Tanzania. Katika kukua kwenye tasnia ya habari mwaka 2015 The Islamic Foundation ilianzisha Gazeti Imaan ambalo sasa linapatikana maeneo mengi nchini.

Mpaka kufkia mwaka 2017 The Islamic Foundation ilikuwa na jumla ya Idara 8 ambazo ni; Idara ya Da’awa, Yatima, Elimu, Habari, Maafa, Usafrishaji, Miradi na Idara ya Fedha.



from TIF http://bit.ly/2VfIBVY
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...