Translate

Jumamosi, 29 Desemba 2018

Mafunzo ya Swalah - Tashahhud katika Rakaa´ ya tatu na ya nne

 MAFUNZO  YA  SWALAH -  TASHAHHUD KATIKA SWALAH ZENYE RAKAA 3 & 4




Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh


Naam basi ikiwa swalah ni ya Rakaa´ tatu, kama Maghrib, au ya Rakaa´ nne kama Dhuhr, ´Aswr na ´Ishaa basi Mswaliji atasoma Tashahhud iliyotanguliwa kutajwa punde tu [baada ya Rakaa´ mbili] pamoja na kumswalia Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) halafu atasimama hali ya kujisaidiza kwa kushika mapaja yake na wakati huo huo ainyanyue mikono yake sawa na mabega yake na huku aseme"Allaahu Akbar" na aiweke mikono yake juu ya kifua chake - kama tulivyotangulia hapo juu - na asome "al-Faatihah" peke yake.

Baadhi ya nyakati katika swalah za Rakaa´ tatu na nne baada ya kusoma "al-Faatihah"akisoma Suurah nyingine ni sawa.

Kumethibiti yanayofahamisha hivo kutoka kwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia Hadiyth ya Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh).

Endapo ataacha kumswalia Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya Tashahhud ya kwanza ni sawa. Kwa sababu imependekezwa na sio jambo la wajibu katika Tashahhud ya kwanza.

Baada ya Rakaa´ ya tatu atakaa Tashahhud [ya mwisho] ikiwa ni Maghrib na [atakaa Tashahhud] baada ya Rakaa´ ya nne ikiwa ni Dhuhr, ´Aswr na ´Ishaa - kama ilivyotangulia katika swalah za Rakaa´ mbili - kisha amswalie Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aombe kinga kutokamana na adhabu ya Moto, kaburi, fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal na akithirishe kuomba du´aa, kama yalivyotangulia hayo katika swalah ya Rakaa´ mbili.

Lakini katika kikao hichi anatakiwa kukaa kitako cha Tawarruk. Nacho ni kuuweka mguu wake wa kushoto chini ya mguu wake wa kulia na makalio yake ayakaze juu ya ardhina wakati huo huo mguu wake wa kulia awe ameusimamisha kutokamana na Hadiyth ya Abu Humayd juu ya hilo.


Kisha atoe Salaam upande wa kulia na wa kushoto hali ya kusema: "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah."


Halafu amuombe Allaah maghfirah mara tatu.

Baada ya hapo atasema: }

 ال نت ال الم منك ال الم تبا كت ا اجلالل اإلك ام

 "Allaahumma antas-Salaam, wa minkas-Salaam, tabaarakta yaadhal-Jalaal wal-Ikraam." 

"Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umetukuka ewe Mwenye utukufu na Mwenye kustahilki kuheshimika."  Muslim (591), at-Tirmidhiy (300), Abu Daawuud (1512), Ibn Maajah (928), Ahmad (05/280) na ad-Daarimiy (1348). 


Yaani kabla ya kuwaelekea watu iwapo huyo mswaliji atakuwa atakuwa ni imamu.

Kisha baada ya hapo aseme:

 ه } حده ال ش يك لو، لو امل ك لو احل د ى ع ىكل شي دي ، ال ال مانع ملا عطيت ال معطي ملا منعت ال ينفع ا ال لو ال اّلل ه خم ل لو ال نعبد ال ه لو النع ة لو الفضل لو الثنا احل ن ال لو ال اّلل ه اجلد منك اجلد، ال ح ل ال ة ال ابهلل، ال لو ال اّلل الدين ل ك ه ال ا ن {

"Laa ilaaha illa Allaah, wahdahuu laa shariyka lah, lahul-Mulk wa lahul-Hamd wa huwaa ´alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa hawla wa laa quwwatah illa billaah. Allaahumma laa maaniy´ limaa a´twayt, wa laa mu´twiya limaa mana´t, wa laa yanfau´ dhal jaddi mink al-Jadd. Laa hawla wa laa quwwatah illa billaah, laa ilaaha illa Allaah, wa laa na´abudu illa iyyaah, lahun-Ni´mah wa lahulFadhwl, wa lahuth-Thanaa´ al-Hasan. Laa ilaaha illa Allaah, mukhliswiyna lahud-Diyn, wa lau karihal-Kaafiruun."

"Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa peke yake hana mshirika, ufalme ni wa Kwake na himdi ni Zake Naye juu ya kila jambo ni muweza. Hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Ee Allaah! Hapana awezae kukizuia ulichokitoa na kukitoa ulichokizuia - wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani Kwako wewe ndio utajiri. Hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah, hatumuabudu mwengine asiyekuwa Yeye, neema na fadhila na sifa nzuri zote ni Zake. Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kumtakasia Yeye dini ijapokuwa watachukia makafiri."Al-Bukhaariy (808), Muslim (593), an-Nasaa´iy (1341), Abu Daawuud (1505), Ahmad (04/250) na ad-Daarimiy (1349).



Kisha Aseme "Subhaan Allaah" mara thelathini na tatu, "Alhamdu lillaah" mara thelathini na tatu, "Allaahu Akbar" mara thelathini na tatu kisha atimize mia kwa kusema"Laa ilaaha illa Allaah illa Allaah, wahdahuu laa shariyka lah, a wa lahulHamd wa huwaa ´alaa kulli shay-in Qadiyr."

Baada ya hapo anaweza akasoma Aayat-ulKursiy, Suurah "al-Ikhlaasw", "al-Falaq" na "an-Naas". Afanye hivi baada ya kila swalah.

Imependekezwa kukariri Suurah hizi mara tatu-tatu baada ya swalah ya Fajr na Maghrib. Kumepokelewa Hadiyth juu ya hayo kutoka kwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Adhkaar zote hizi ni Sunnah na sio faradhi.


Imependekezwa kwa kila Muislamu mwanaume na mwanamke kuhifadhi Rakaa´ kumi na mbili anapokuwa katika hali isiyokuwa ya usafiri.

Nazo ni kuswali kabla ya Dhuhr Rakaa´ nne na Rakaa´ mbili baada yake,

Rakaa´ mbili baada ya Maghrib, Rakaa´ mbili baada ya ´Ishaa na Rakaa´ mbili kabla ya Fajr.

Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizihifadhi katika hali isiyokuwa ya usafiri. Kuhusu anapokuwa katika hali ya usafiri alikuwa haziswali isipokuwa Sunnah ya Fajr na Witr.

Hakika hizi mbili Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizihifadhi katika anapokuwa safarini na asipokuwa safarini.

Lililo bora ni kuziswali Raatibah hizi na Witr nyumbani. Lakini hata hivyo akiziswali msikitini pia ni sawa. Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Swalah bora ya mtu ni ile anayoswali nyumbani kwake isipokuwa zile za faradhi."Al-Bukhaariy (689), Muslim (1301) na at-Tirmidhiy (412).


Kuhifadhi swalah hizi ni miongoni mwa sababu zinazompelekea mtu kuingia Peponi. Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Anayeswali Rakaa´ kumi na mbili mchana na usiku, basi Allaah atamjengea nyumba Peponi." Muslim (1198-1199), Abu Daawuud (1059) na an-Nasaa´iy (1773).

Endapo ataswali Rakaa´ nne kabla ya ´Aswr, Rakaa´ mbili kabla ya Maghrib na Rakaa´ mbili kabla ya ´Ishaa ni jambo zuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Atakayehifadhi Rakaa´ nne kabla ya Dhuhr na Rakaa´ nne baada yake, basi Allaah (Ta´ala) atamharamishia Moto." At-Tirmidhiy (393), Abu Daawuud (1077) na Ahmad (25547).


Ina maana ya kwamba akizidisha Rakaa´ mbili baada ya Dhuhr - kwa sababu Sunnah ya Raatibah ni nne kabla yake na mbili baada yake - basi atakuwa amefikia kile kilichotajwa katika Hadiyth ya Umm Habiybah (Radhiya Allaahu ´anhaa).



Na  Allaah  anajua  zaidi


Ukiwa na Swali lolote  kuhusu Somo hili tafadhali wasiliana na Imaam Masjid Tawbah kwa namba 0714974397 au Email : http://bit.ly/2LDVR23

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2s2ayDj
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...