Swali:
Je, inatosha kusema “Bismillaah” bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja.
Jibu:
Kusema “Bismillaah” wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume (´alayhis-Swalaat was-Salaam).
Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”.
Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja “Bismillaah Allaahu Akbar”. Hii ndio Sunnah. Na lau atasema “Bismillaah” yatosha.
Haifai kwake kukusudia kuacha kusema “Bismillaah”. Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali.
Lakini haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo limependekezwa na wala sio la wajibu.
Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah, ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio bora zaidi.
Mhusika : Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Marejeo : Nuur ´alaad-Darb
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2ApSLuj
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni