Swali:
Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa ´Abaa´ah ya mapambo, anaweka ´Abaa´ah mabegani na kuvaa suruwali?
Jibu:
Naam, kwanza kabisa Suruwali haijuzu kwa mwanamke.
Kwasababu Suruwali sio vazi la mwanamke.
Mwanamke anatakiwa kuvaa vazi pana, lenye kusitiri na lililo la wasaa.
Kwahiyo haijuzu kwake kuvaa mavazi ya kubana.
Suruwali ni vazi la kubana. Haijuzu kwake.
´Abaa´ah la mapambo halijuzu. ´Abaa´ah ni kwa ajili ya kujisitiri. Sio kwa ajili ya kujipamba. ´Abaa´ah halitakiwi kuwa na mapambo na michoro.
Wakati anapotoka ´Abaa´ah anatatakiwa kuliweka juu ya kichwa. Hata hivyo hakuna neno akaliweka mabegani mwake anapokuwa nyumbani au pamoja na wanawake wenzake.
Marejeo : Liqaa'-ul-Jumu´ah bit-Twaa'if
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2EX5WWC
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni