Translate

Jumamosi, 29 Desemba 2018

Ibn Taymiyyah kuhusu swalah ya ´Iyd

Swali: Kule wanawake waliotoka kuvunja ungo na wanawake wenye hedhi kuhudhuria swalah ya ´Iyd ni dalili inayofahamisha juu ya kwamba swalah ya ´Iyd ni wajibu?

Jibu: Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametoa dalili hii kuonyesha kwamba swalah ya ´Iyd ni wajibu na kwamba swalah hiyo ni fadhi. Amesema kwamba dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kuwatoa nje wanawake, wanawake wenye hedhi na wale waliotoka kuvunja ungo. Akaambiwa: “Ee Mtume wa Allaah! Vipi ikiwa mwanamke hana Jilbaab?” Akasema: “Dadake amuazime Jilbaab yake na atoke nje.” Kwa lengo la kushuhudia ´Iyd, ahudhurie kheri na asikilize Dhikr. Aliamrisha watolewe nje wale mateka, wanawake wenye hedhi na wale waliotoka kuvunja ungo. Mwanamke akiwa hana Jilbaab basi aazime kutoka kwa dada yake. Mfano wake ni hizi ´Abaa´ah za leo. Hii ni dalili inayofahamisha juu ya kwamba swalah ya ´Iyd ni wajibu. Kwa ajili hiyo Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) ametumia hoja kwa maamrisho haya juu ya kwamba swalah ya ´Iyd ni faradhi kwa kila mtu. Wapo wanachuoni waliosema kwamba ni faradhi kwa baadhi ya watu tu. Baadhi ya wanachuoni wengine wakasema kuwa ni sunnah iliokokotezwa. Kwa hiyo kuna maoni matatu.



from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2SpmeLL
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...