Translate

Jumamosi, 29 Desemba 2018

Mwanamke ni lazima ajifunike Kichwa akiwa Nyumbani kwake ..?

Swali


WANAMKE ANAPOKAA KICHWA WAZI NDANI YA NYUMBA YAKE MALAIKA WEMA HAWAINGII? HATA KAMA YUKO NA MAHARIMU ZAKE AU YUKO PEKE YAKE NAOMBA UFAFANUZI



Jibu


Ama kuhusu swali la kwanza hakuna tatizo lolote kwa mwanamke kuwa kichwa wazi akiwa mbele ya maharimu zake kwani hiyo ni sehemu ambayo yaweza kuonekana bila wasiwasi wowote. 

Allaah Aliyetukuka Anatueleza:

"Wala wasidhihirishe viungo vyao ila vinavyodhihirika. Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au watoto wa kaka zao, au wana wa dada zao, …" (24: 31).

Bila shaka, kichwa ni lazima kifunikwe ikiwa yu mbele ya waume wasio maharimu zake au akitoka nje kwa shughuli zake.

Na Allaah Anajua zaidi


from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Tc6ZWy
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...