SWALI:
Je mtoto aweza kumuombea dua gani mzazi wake hali ya kuwa huyo mzazi si muislaam?
JIBU:
Ikiwa mzazi huyo yuko haai unaweza ukamuombea Du'aa ili Mwenyezi Mungu amuongoze na aulainishe moyo wake ili aweze kuingia kwenye Uislaam
Na ikiwa mzazi huyo ameshafariki hali yakuwa hakusilimu na kafa kwenye ukafiri hapo tena haifai kumuombea Du'aa na wala kumuombea (Maghufira) msamaha kwasabubu ameshakuwa ni mtu wa motoni milele na ndio ahadi ya Mwenyezi Mungu
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu
قَالَ اللهُ تَعَالَى ﴿ اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّهُ لَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴾
Waombee msamaha au usiwaombee. Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotofu.
(Surat At-Tawba Aya-80)
Na vile vile Mwenyezi Mungu anatuambia tena kwa kututahadharisha kutokuwaombea Du'aa wakati ambao wameshafariki
قَالَ اللهُ تَعَالَى ﴿ مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴾
Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni.(Surat At-Tawba Aya-113)
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2BPgWCl
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni