Translate

Jumatatu, 31 Desemba 2018

Kuzidisha kheri

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh


Baada ya Allaah Kufaradhisha kufunga Ramadhaan, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawashaji´isha kuifuatisha Ramadhaan kwa kufunga siku zile za Shawwaal.

Amefanya hivi ili ujira wao uweze kuwa mkubwa na ili waweze kulipwa kama aliyefunga mwaka mzima. Abu Ayyuub al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayefunga Ramadhaan na akaifuatisha kwa kufunga siku sita za Shawwaal, ni kama amefunga mwaka mzima.” Haafidhw al-Mundhiriy amesema: “Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na at-Twabaraaniy amezidisha na kusema:

“Nilisema: “Kila siku hulipwa kwa kumi.” Akasema: “Ndio.” Wamepokezi wake ni wapokezi sahihi.


Mwaka hauwezi kuzidi siku 360. Siku sita za Shawwaal zikiwekwa katika Ramadhaan nzima na kila siku moja inalipwa kwa thawabu kumi (kwa kuwa tendo moja zuri linalipwa mara kumi) Waislamu wanazingatiwa kuwa wamefunga mwaka mzima. Kwa ajili hiyo amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ni kama amefunga mwaka mzima.” Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah. Himdi na shukurani zote ni za Allaah zisizohesabika.


Kutoka kheri kwenda nyingine 


Katika fadhila za Allaah kwa waja Wake ni kwamba Amewasahilishia njia ambazo zinawanyanyua katika daraja.

Vile vile Amewajaalia daima mafungamano yenye nguvu na ´ibaadah za Allaah. Baada ya masiku na usiku za Ramadhaan (ambapo ndani yake Allaah Anayasamehe madhambi, Anazinyanyua daraja na kuyafuta makosa) kuisha, viumbe wanakuwa wamemkurubia Mola Wao.

Baada ya hapo kidogo huanza miezi ya Hajj, ambapo ndani yake inaendewa Nyumba Tukufu ya Allaah. Siku ya ´Iyd-ulFitwr, ambayo ni ile siku ya kwanza ya Shawwaal, ndio siku ya kwanza ya miezi ya Hajj.

Allaah (Ta´ala) Amesema juu yake:

 ٌت ا َ لُوم ْ َّمع ٌ ر ُ ْشه ج أَ ُّ َ ۚ ا ْْل ج ِّ َ اَل ِِف ا ْْل َ د ََّل جِ َ وَق و ُ ُس ََّل ف َ َ َث و ف َ ََل ر ج ف َّ َ ن ا ْْل َّ ِه ي ِ َ َض ف َر ن ف َ َم ۚ لُوا ف َ ْع َف ا ت َ م َ و ُ ه َّ الل ُ ه ْ لَم ْ ع َ ي ٍ ْ َْي ْ خ ن ۚ ى ِ م َ ْو َّ ق الت ِ زاد الَّ َ ر ْ ي َ ن خ َّ ِ إ َ وا ف ُ ود َّ َ َز ت َ ۚ و َ ا أُوِِل اْْلَلْب َ ي ُونِ َّ ق ات َ ِب و ا

“Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji, basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote mlifanyalo katika ya kheri Allaah Analijua. Na jitengenezeeni akiba. Na hakika bora ya akiba ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili!” 02:197


Katika Ramadhaan ndio kumeteremshwa Qur-aan iliyobarikiwa. Katika Ramadhaan milango ya Pepo inafunguliwa na milango ya Moto inafungwa.


Katika siku za Swawm Mashaytwaan wanafungwa. Allaah (Ta´ala) Amesema kuhusu siku hizi katika Hadiyth al-Qudsiy: “Kila ´amali ya mwanaadamu inalipwa mara kumi. Isipokuwa Swawm tu. Ni Yangu na Mimi ndio nitailipa.” Wakati masiku haya hayanaisha, kunakuja masiku ya Hajj. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu masiku haya:

“Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo vichafu, atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake.” Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengine.

Amesema pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “'Umrah hadi 'Umrah ni kafara [kufutiwa dhambi] baina yao, wakati Hajj iliyokubaliwa haina jazaa isipokuwa ni Pepo.” Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengine.

Muislamu hakaribii kukamilisha mmoja katika misimu ya Aakhirah, isipokuwa unakuja mwingine mpya. Hili linaendelea ili awe kila siku ni mwenye kumwabudu Mola Wake Aliyemuumba baada ya kukosekana na Akamjazia neema Zake za dhahiri na zilizojificha.


Na  Allaah  anajua  zaidi

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Vi6tbD
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...