Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma Tashahhud kila baada ya Rak´ah mbili[1]. Kitu cha kwanza anachosema punde tu baada ya kukaa chini:
التحيات لله
“Maadhimisho yote yanamstahiki Allaah.”[2]
Akisahau (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Tashahhud ya kwanza, basi huleta Sujuud-us-Sahuw[3]. Aliamrisha Tashahhud na akasema:
“Mnapokaa chini kila baada ya Rak´ah mbili basi semeni:
…التحيات لله
“Maadhimisho yote yanamstahiki Allaah… “
na chagueni du´aa inayokupendezeni na mumuombe Allaah (´Azza wa Jall).”[4]
Katika upokezi mwingine imekuja:
“Semeni katika kila kitako:
…التحيات لله
“Maadhimisho yote yanamstahiki Allaah… “[5]
Vivyo hivyo alimwamrisha yule mtu aliyeswali kimakosa, kama ilivyotangulia punde tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwafunza Tashahhud kama anavyowafunza Suurah kutoka katika Qur-aan[6]. Sunnah ni kuisoma kimyakimya[7].
[1] Muslim na Abu ´Awaanah.
[2] al-Bayhaqiy kupitia kwa ´Aaishah kwa cheni ya wapokezi nzuri, amesema Ibn-ul-Mulaqqin (2/28).
[3] al-Bukhaariy na Muslim. Imetajwa katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (338).
[4] an-Nasaa’iy, Ahmad na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1/25/3) kwa cheni Swahiyh. Udhahiri ni kwamba imewekwa katika Shari´ah kuomba katika kila Tashahhud hata kama sio Rak´ah ya mwisho. Haya pia ndio maoni ya Ibn Hazm (Rahimahu Allaah).
[5] an-Nasaa’iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
[6] al-Bukhaariy na Muslim.
[7] Abu Daawuud na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2EYoAhJ
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni