MAFUNZO YA SWALAH - KIKAO KATIKA TASHHUD YA KWANZA NA PILI
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Naam Basi Mswaliji ikiwa swalah ni ya ni Rakaa´ mbili, kwa mfano swalah ya Fajr, Ijumaa na ´Iyd, baada ya kuinuka kutoka katika Sajdah ya pili atakaa hali ya kusimamisha mguu wake wa kulia na wakati huo huo ameulaza mguu wake wa kushoto na huku ameuweka mkono wake wa kulia juu paja lake la kushoto na amekunja vidole vyake vyote isipokuwa kidole cha shahaadah.
Kidole hicho anatakiwa kuashiria Tawhiyd.
Mswaliji anatakiwa akikunje kidole cha mwisho na kidole cha pete kisha akakutanisha kidole gumba na kidole kirefu halafu akaashiria kidole cha shahaadah ni bora zaidi. Sifa zote mbili zimethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Lililo bora zaidi afanye hili wakati fulani na hili wakati mwingine.
Mswaliji aweke mkono wake wa kushoto juu ya paja na goti lake la kushoto kisha asome Tashahhud katika kikao hichi:
} ال يات هلل الل ات الطيبات، ال الم ع يك ي ا النيب محة هللا ب كاتو، ال الم ع ينا ع ى عباد هللا اللاحل ، ش د ن ال لو ال ا عبده و لو، مث يق ل ال صل ع ى دمحم ع ى ل دمحمك ا ص يت ع ى ب اىي ل ب اىي نك محيد جميد، اب ك ً ش د ن حم د ه اّلل ع ى دمحم ع ى ل دمحم ك ا اب كت ع ى ب اىي ل ب اىي نك محيد جميد {
"At-Tahiyyaatu lillaahi was-Swalawaatu wat-Twayyibaat. as-Salaam ´alayka ayyuha an-Nabiyy wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh. as-Salaam ´alaynaa wa ´alaa ´ibaadi llaahi as-Swaalihiyn. Ashhaduu allaa ilaaha illa Allaah wa ash-haduu anna Muhammadan ´abduhuu wa Rasuuluh."
"Maamkuzi mema na swalah na mazuri yote ni kwa Allaah. Amani ziwe juu yako, ee Mtume, na rehema za Allaah na baraka Zake. Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wa Allaah walio wema. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja na ni Mtume Wake."
Kisha aseme:
)ال صل ع ى دمحم ، ع ى ل دمحم ، ك ا ص يت ع ى ب اىي ع ى ل ب اىي ، نك محيد جميد ، اب ك ع ى دمحم ، ع ى ل دمحم ، ك ا اب كت ع ى ب اىي ، ع ى ل ب اىي نك محيد جميد(
"Allaahumma swalli ´alaa Muhammad, wa ´alaa aali Muhammad, kamaa swalayta ´alaa Ibraahiym, wa ´alaa aali Ibraahiym, innaka hamiydun majiyd, wa baarik ´alaa Muhammad, wa ´alaa aali Muhammad, kamaa barrakta ´alaa Ibraahiym, wa ´alaa aali Ibraahiym, innaka hamiydun majiyd."
"Ee Allaah! Mswalie Muhammad na familia ya Muhammad kama Ulivyomswalia Ibraahiym na familia ya Ibraahiym - hakika Wewe ni muhimidiwa mtukufu - na mbariki Muhammad na familia ya Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na familia ya Ibraahiym - hakika Wewe ni muhimidiwa mtukufu." Al-Bukhaariy (797), Muslim (402), at-Tirmidhiy (1105), an-Nasaa´iy (1298), Abu Daawuud (968), Ibn Maajah (899), Ahmad (01/428) na adDaarimiy (1340).
Halafu aombe kinga dhidi ya mambo mane kwa kusema: }
ال ين ع بك من ع اب ن من ع اب القرب من نة احمليا امل ات من نة امل يح الد ال {
"Allaahumma inniy a´udhubika min ´adhabi jahannam, wa min ´adhab al-Qabr, wa min fitnat-ilMahyaa wal-Mamaat, wa min fitnat-il-Masiyh ad-Dajjaal."
"Ee Allaah! Naomba unikinge kutokamana na adhabu ya Moto na kaburi na kutokamna na fitina za uhai na kifo na kutokamana na fitina za al-Masiyh adDajjaal." Al-Bukhaariy (1311), Muslim (588), at-Tirmidhiy (3604), an-Nasaa´iy (5513), Abu Daawuud (983), Ibn Maajah (909), Ahmad (02/454) na adDaarimiy (1344).
Kisha aombe anachokitaka katika kheri za duniani na Aakhirah. Akiwaombea wazazi wake wawili au waislamu wengine du´aa ni sawa.
Ni mamoja iwe swalah ni ya faradhi au ya Sunnah. Halafu atoe Salaam upande wa kulia na wa kushoto hali ya kusema:
"as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah."
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2ERNfUm
via IFTTT
Translate
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh YAFUATAYO NI MAJINA YA MASWAHABA WANAWAKE (RADHI ZA ALLAAH...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
Assallaaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Naam, Ndugu zangu katika Imaani, Siku chache zimebaki kwa ajili ya Vijana wetu wanaosoma Elim...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni