Translate

Ijumaa, 28 Desemba 2018

Mafunzo ya Swalah - Kikao baina ya Sijda

                    MAFUNZO  YA  SWALAH  -  KIKAO  BAINA  YA  SIJDA



Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh



Naam,Mswaliji anyanyue kichwa chake na huku akisema "Allaahu Akbar" na auinamishe mguu wake wa kushoto na auikalie na wakati huo huo asimamishe mguu wa kulia na aweke mikono yake juu ya mapaja na magoti yake na aseme:

"Rabb Ighfir liy, wahdiniy, warhamniy, warzuqniy, wa ´aafiniy na wajburniy."


"Ee Mola! Nisamehe, uniongoze, unihurumie, uniruzuku, nipe afya na uniunge."at-Tirmidhiy (284), Abu Daawuud (850) na Ibn Maajah (898).



Mswaliji anatakiwa awe na utulivu katika kikao hichi.


Asujudu Sijda ya pili na huku akisema "Allaahu Akbar" kisha afanye yale yale aliyofanya katika Sajdah ya kwanza.


Ainue kichwa chake na huku akisema "Allaahu Akbar" na akae kikao khafifu kama mfano wa kikao baina ya Sajdah mbili. Hiki huitwa kuwa ni "kikao cha kustarehe" ambacho kimependekezwa kwa mujibu wa maoni sahihi ya wanachuoni. Endapo atakiacha hakuna neno.

Katika kikao hichi hakuna Dhikr wala du´aa. Kisha asimame/apande kwenda katika Rakaa´ ya pili hali ya kujisaidiza kwa kushika mapaja - ikiwa kuna urahisi wa kufanya hivo - la sivyo ajisaidize kwa ardhi. Halafu asome "al-Faatihah" na kilicho chepesi kwake katika Qur-aan baada ya al-Faatihah.

Ataendelea kufanya kama alivyofanya katika Rakaa´ ya kwanza.



Na  Allaah anajua  zaidi

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2TgbRKd
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...