MAFUNZO YA SWALAH - KURUKUU
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Rukuu´, kuinuka kutoka katika Rukuu´ na yenye kuhusiana na Rukuu
Mtu anapotaka kurukuu na wakati huo huo aseme "Allaahu Akbar" na huku amenyanyua mikono yake sawa na mabega au masikio yake.
Vilevile akiweke kichwa chake sawa na mgongo wake, mikono yake aiweke kwenye magoti yake na hali ya kuwa ameachanisha vidole vyake. Afanye yote haya huku ametulia na aseme mara tatu maneno haya:
"Subhaana Rabb al-A´dhwiym.""Ametakasika, Mola mtukufu
Bora zaidi akariri mara tatu au zaidi. Pamoja na kusema hivyo imependekezwa vilevile kuongezea juu yake:
"Subhaanak Allaahumma wa bihamdik. Allaahumma Ighfir liy."
"Utakasifu na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe." Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy (4683), Muslim (484), an-Nasaa´iy (1122), Abu Daawuud (877) na Ibn Maajah (889).
Baada ya hapo, Mswaliji anatakiwa anyanyue kichwa chake kutoka kwenye Rukuu´ na wakati huo huo ni mwenye kunyanyua mikono yake sawa na mabega yake au masikio yake na huku akisema:
"Sami´ Allaahu li man hamidah"
"Allaah anamsikia yule anayemuhimidi." Imepokelewa na Imaam al-Bukhaariy (657), Muslim (411), at-Tirmidhiy (361), an-Nasaa´iy (832), Abu Daawuud (601), Ibn Maajah (1238) na ad-Daarimiy (1256).
Atasema hivi sawa awe ni imamu au anayeswali peke yake. Kisha aseme wakati amesimama: }
ا طيباً مبا ًكا يو مل ال ا ات مل األ ض مل ما بين ا مل ما شئت من شي بعد ً اكثري بنا لك احل د محد ً
"Rabbanaa wa lak al-Hamd, hamdan kathiyran twayyiban mubaakan fiyh, mil-a as-samawaat, wa mil-a al-Ardhw, wa mil-a maa baynahumaa, wa mil-a maa shi´ta min shay-in ba´du."
"Ee Mola! Sifa na himdi zote ni Zako. Himdi zilizo nyingi, nzuri na zilizo na baraka - zimejaa mbingu, zimejaa ardhi na zimejaa vilivyomo baina yake na zimejaa kwa Ulichokitaka baada yake."
Baada ya hapo akiongezea juu yake: }
ىل الثنا اجملد ح ما ال العبد ك نا لك عبد، ال ال مانع ملا عطيت ال معطي ملا منعت ال ينفع ا اجلد منك اجلد {
"Ahluth-Thanaa´ wal-Majd, ahaqqu maa qaal al-´Abd wa kullunaa laka al-´Abd. Allaahumma laa maaniy´ limaa a´twayt, wa laa mu´twiya limaa mana´t, wa laa yanfau´ dhal jaddi mink al-Jadd."
"Wewe ni mstahiki wa sifa na utukufu, ni kweli alivyosema mja Wako na sote ni waja Wako. Ee Allaah! Hapana awezae kukizuia ulichokitoa na kukitoa ulichokizuia - wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani Kwako wewe ndio utajiri." Muslim (477), an-Nasaa´iy (1068), Abu Daawuud (847), Ahmad (03/87) na ad-Daarimiy (1313).
ndio bora zaidi. Hilo limethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika baadhi ya Hadiyth Swahiyh.
Kuhusu maamuma wakati anapoinuka anatakiwa kusema:
"Rabbanaa wa lakal hamd... "
"Ee Mola! Sifa na himdi zote ni Zako."
Imependekezwa kwa imamu na maamuma wote wawili warudishe mikono yao juu ya vifua vyao. Alikuwa katika hali hiyo kabla ya kurukuu. Kumepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yenye kufahamisha hivo kupitia Hadiyth hya Waa-il bin Hajar na Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anhumaa).
Na Allaah anajua zaidi
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2ER71PL
via IFTTT
Translate
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
SWALI: Assalaam alaykum Naomba maana ya majina yeyote tuwapao watoto wetu AU mnielekeze wapi naweza kupata labda katika kitabu cha fas...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni