RIBA NA HUKMU ZAKE
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad.
Maana ya Riba
Ni Neno la Kiarabu ambalo lina maana mbili, yaani lina maana kilugha na pia lina maana Kisheria kama ifuatavyo
1⃣Riba katika lugha ya kiarabu maana yake ni ziada.
2⃣Ama katika lugha ya elimu ya fiq-hi maana ya neno 'Riba', ni ile ziada
Riba ina maana ya ziada anayopewa mdeni anapolipwa deni lakekwa mapatano waliyopatana kuanzia awali ya mkopo.
Mfano umeenda kwa Ally kumkopa Pesa Shilingi 10,000/= na akakuambia kwamba umrejeshee Shilingi 11,000/= basi hiyo Shilingi 1,000/= iliyoongezeka ni Riba.
Hukmu za Riba
✅Naam, Ndugu zangu katika Imaani Riba kwa Ujumla ni HARAMU
➡Hakuna Riba Ndogo wala Riba Kubwa, Ikiwa ni Riba kwa namna yoyote ile basi hiyo inakuwa ni Riba tu hata ikiwa ni Ndogo kiasi gani kwa ujumla hiyo itabaki kuwa Riba.
➡Na Allaah (Subhaana wa Taala) Katika Qur'an Tukufu ametuharamishia na kutuhadhalisha na Riba.
➡Allaah (Subhaana wa Taala) Ameharamisha kuchukua na kutoa ribaa katika njia zake zote.
➡Allaah (Subhaana wa Taala) Anasema: “Allaah Amehalalisha biashara na kuiharamisha ribaa”
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 275.
➡Na amesema Allaah (Subhaana wa Taala) kwamba⤵
“Enyi Mlioamini! Mcheni Allaah, na acheni yaliyobakia katika ribaa, ikiwa mmeamini. Na kama hamtafanya hivyo, basi fahamuni mtakuwa mmetanganza vita na Allaah na Mtume Wake”
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 278 – 279.
Al-Hadiythi kuhusu Uharamu wa Riba
Hadiythi hizi zipo kwenye Buluwgh Al-Maraam,Kitab cha Biashara ,Mlango wa Riba
عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {لَعَنَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ آكِلَ اَلرِّبَا، وَمُوكِلَهُ، وَكَاتِبَهُ، وَشَاهِدَيْهِ، وَقَالَ: " هُمْ سَوَاءٌ "} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَلِلْبُخَارِيِّ نَحْوُهُ مِنْ حَدِيثِ أَبِي جُحَيْفَةَ
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amemlaani mlaji ribaa, mwakilishi wake, mwandishi wake, na mashahidi wake wawili na akasema: “Wote wako sawa.”
↪Imepokelewa na Imaam Muslim
✅Kwa maana ya kwamba Ribaa ni haraam kwa dalili zilizo wazi kabisa katika Qur-aan. Yeyote atakayetoa mkopo kwa sharti la ribaa, na atakayepokea, mwandishi wake na shahidi wake, wote wamelaaniwa.
➡Na katika Al-Bukhaariy amepokea kama hiyo katika Hadiyth ya Abuu Juhayfah
وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {اَلرِّبَا ثَلَاثَةٌ وَسَبْعُونَ بَابًا أَيْسَرُهَا مِثْلُ أَنْ يَنْكِحَ اَلرَّجُلُ أُمَّهُ، وَإِنَّ أَرْبَى اَلرِّبَا عِرْضُ اَلرَّجُلِ اَلْمُسْلِمِ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ مُخْتَصَراً، وَالْحَاكِمُ بِتَمَامِهِ وَصَحَّحَهُ
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Ribaa ina milango sabini na tatu mwepesi wake ni mfano wa mtu kumuowa mama yake. Kwa hakika ribaa kubwa zaidi ni mtu kuchafua heshima ya Muislam.”
↪Imetolewa na Ibn Maajah kwa mukhtasari, na Al-Haakim ameipokea kwa ukamilifu na akaisahihisha.
وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ، وَأَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ اِسْتَعْمَلَ رَجُلًا عَلَى خَيْبَرٍ، فَجَاءَهُ بِتَمْرٍ جَنِيبٍ، فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَكُلُّ تَمْرِ خَيْبَرَ هَكَذَا ؟ " فَقَالَ: لَا، وَاَللَّهِ يَا رَسُولَ اَللَّهِ، إِنَّا لَنَأْخُذُ اَلصَّاعَ مِنْ هَذَا بِالصَّاعَيْنِ وَالثَّلَاثَةِ فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ " لَا تَفْعَلْ، بِعِ اَلْجَمْعَ بِالدَّرَاهِمِ، ثُمَّ اِبْتَعْ بِالدَّرَاهِمِ جَنِيبًا} وَقَالَ فِي اَلْمِيزَانِ مِثْلَ ذَلِكَ. مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِمُسْلِمٍ: "وَكَذَلِكَ اَلْمِيزَانُ "
Kutoka kwa Abuu Sa’iyd na Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) wamesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimtawalisha mtu Khaybar,[5] akamjia na tende nzuri. Akasema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Tende zote za Khaybar ziko hivi?” Akasema: “Hapana. Wa-Allaahi Ee Rasuli wa Allaah! Hakika sisi huchukuwa pishi moja ya tende hizi kwa pishi mbili, au tatu (duni ya hizi).” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Usifanye hivyo, uza tende duni kwa dirhamu kadhaa kisha ununue tende nzuri kwa dirhamu kadhaa.” Na katika mizani alisema kama hivyo.”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy, Muslim
وَعَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: {سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ سُئِلَ عَنِ اِشْتِرَاءِ اَلرُّطَبِ بِالتَّمْرِ. فَقَالَ: أَيَنْقُصُ اَلرُّطَبُ إِذَا يَبِسَ ؟ " قَالُوا: نَعَمَ. فَنَهَى عَنْ ذَلِكَ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلْمَدِينِيِّ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Sa’d bin Abiy Waqqaasw[19] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiulizwa kuhusu kununua tende mbivu kwa tende kavu, akasema: ‘Je mbivu hupungua zinapokauka?” Wakasema: “Ndio.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akakataza kufanya hivyo.”
↪Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha Ibn Al-Madiyniyy, At-Tirmidhiyy, Ibn Hibbaan na Al-Haakim.
Hadiythi zipo nyingi sana Rejea Kitab nilichokitaja hapo juu kuzisoma zaidi
AINA ZA RIBA
➡Naam kuna aina kuu mbili za riba ambazo ni ‘Riba An Nasiyah’ na ‘Riba Al Fadhil’.
✅Naam, Ama katika zama za ujahiliya aina ya kwanza tu ilijulikana kama riba ingawa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alipokuja alibainisha aina ya pili ya riba.
➡Kwakua Riba An Nasiyah ilikuwa ndio aina pekee ya riba inayojulika katika kipindi cha ujahiliya (kabla ya Uislamu),hivyo aina hii ya riba huitwa Riba Al Jahiliya na kwakua pia aina hii ya riba ndio iliyokatazwa moja kwa moja katika Quran, aina hii pia huitwa Riba Al Quran.
1.RIBA AN-NASIYAH
➡Riba An Nasiyah ni ziada anayolipa mtu aliyekopeshwa kwa kushurutishwa na mdai.
➡Yaani kwa mfano mtu akitaka kukopa shilingi elfu, anashurutishwa kulipa shilingi elfu na mia moja zaidi. Sasa zile shillingi miamoja zaidi ndiyo Riba yenyewe.
➡Allaah (Subhaana wa Taala) anatuhimiza kuwa ikiwa mtu anataka kumkopesha mwenzake mwenye shida, basi amkopeshe mkopo mwema bila ya kumuongezea mwenzake dhiki, na kwamba kufanya hivyo ndiyo mali yake mtu inaongezeka baraka itokayo kwa Mola wake, ama unapomkopesha mwenye shida kisha ukachukua faida ya Riba, basi huko ni kumzidishia dhiki mwenzio na pia ni kuiangamiza mali yako na kuiondolea baraka.
➡Riba hii pia inahusisha ziada juu ya deni kwasababu ya kuakhirisha kulipa pale ambapo mkopaji ameshindwa kulipa kwa wakati ambapo huongezewa kiasi cha ziada cha kulipa kwa kushindwa kulipa deni kwa wakati.
✅Hii pia ni haramu, Kwani hukumu za mdaiwa zipo wazi pindi muda wake unapokwisha.
➡Nazo ni amma kumsamehe au kumpa muda zaidi na si kuongeza deni. Allaah(Subhaana wa Taala) anasema⤵
“Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua”
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 280
➡Ama tukija kufunga mlango wa nyuma wa kula riba katika hadith ya Anas ibn Malik (Radhi za Allah ziwe juu yake) Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amekataza mkopeshaji kupokea zawadi kutoka kwa mkopaji, pia katika hadith nyingine ya Anas ibn Malik katika Sunan al-Bayhaqi Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amekataza mkopeshaji kuchukua chakula au kupanda kipando cha mkopaji kama haikuwa ada yao kabla ya kukopeshana.
Ukweli ni kwamba aina hii ya riba imeshika hatamu katika wakati wetu huu nakuwa moja ya sehemu ya msingi ya uchumi na biashara.
➡Mfumo wote wa kifedha umejengwa juu ya riba, kutoka kwenye vyama vya kuweka akiba na kukopa mpaka benki zinazoitwa benki za kibiashara (commercial banks) hujiendesha kwa riba kama chanzo mama cha mapato.
➡Kutoka kwa Abu Hurayrah: Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amesema “Kwa hakika itakuja zama kwa mwanaadamu ambapo kila mtu atakula riba na kama hatofanya hivyo vumbi lake litamfikia”
↪Imepokelewa na Imaam Abu Dawud na Ibn Majah
➡Mfano umeenda kwa Ally kumkopa Pesa Shilingi 10,000/= na akakuambia kwamba umrejeshee Shilingi 11,000/= basi hiyo Shilingi 1,000/= iliyoongezeka ni Riba.

2.RIBA YA AL-FADHIL
➡Riba ya Al-Fadhil (kufadhilisha) ni ile ya kubadilishana pesa kwa pesa au chakula kwa chakula na kuchukuwa zaidi.
➡Kwa mfano mtu anapokwenda kubadilisha dhahabu yenye uzito wa gram kumi kwa ajili ya kupata dhahabu nyengine iliyomvutia zaidi, akalipwa badala yake dhahabu yenye uzito wa gram saba. Hiyo inahesabiwa ni Riba.
➡Inavyotakiwa kwanza mtu aiuze dhahabu ile kwa thamani yake, kisha ainunue dhahabu anayoitaka.
➡Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amesema; "Msiuze Dirham moja kwa Dirham mbili, kwani nakuogopeeni Riba".
Na akasema; "Dhahabu kwa dhahabu, fedha kwa fedha, ngano kwa ngano, chumvi kwa chumvi, mkono kwa mkono, atakayechukua zaidi au kutaka zaidi, kesha kula Riba"
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad na Al-Bukhariy.
➡Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume Muhammad(Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) akiwa amebeba tende.Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) akamwambia; "Tende hii haipatikani kwetu hapa?" Mtu yule akasema; "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tumebadilishana tende yetu pishi moja kwa pishi mbili za tende hizi".
➡Mtume Muhammad (Swallah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) akamwambia; "Hiyo ni Riba, zirudishe, kisha uza tende yetu, halafu nunua tende hizi"
↪Imepokelewa na Imaam Muslim
✅Kwa ujumla ni haramu kuzidisha katika kubadilishana kitu cha jinsi moja.
➡Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amebainisha bidhaa sita ambazo ni ngano, dhahabu, fedha, tende, shairi na chumvi ambapo katika kubadilishana bidhaa ya namna moja hubadilshwa kwa bidhaa ya namna hiyohiyo kwa kipimo cha ujazo au uzito ulio sawa bila kuzingatia tofauti ya ubora iliyopo.
➡Mathalan kilo moja ya tende ya daraja ya juu kwa ubora hubadilishwa kwa kilo moja ya tende ya daraja ya chini yenye ubora duni na si vinginevyo.
➡Au anaehitaji tende za daraja ya juu auze tende zake zenye ubora duni katika soko na atumie thamani hiyo kununua tende za daraja ya juu katika ubora.
➡Na bidhaa hizi hubadilishwa hapo kwa papo, mkono kwa mkono (spot transaction).
➡Na inaruhusiwa kuzidisha ikiwa vitu vya jinsi mbalimbali.
Mfano
Mfano kilo mbili za ngano kwa kilo moja ya tende. Lakini hairuhusiwi kuahirisha katika vitu vya aina hii, yaani inatakiwa mkono kwa mkono.
✅Kuharamishwa aina hii ya riba kuna kufunga mlango wa nyuma wa kula riba na aina yoyote ya dhuluma, udanganyifu na hadaa katika kubadilishana bidhaa.
Na Allaah anajua zaidi
➡Mfano umeenda kwa Ally kumkopa Pesa Shilingi 10,000/= na akakuambia kwamba umrejeshee Shilingi 11,000/= basi hiyo Shilingi 1,000/= iliyoongezeka ni Riba.
https://ift.tt/2Kfi0XM i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni