Translate

Alhamisi, 4 Aprili 2019

Aina za Riba

                                                      1.RIBA  AN-NASIYAH


➡Riba An Nasiyah ni ziada anayolipa mtu aliyekopeshwa kwa kushurutishwa na mdai.

➡Yaani kwa mfano mtu akitaka kukopa shilingi elfu, anashurutishwa kulipa shilingi elfu na mia moja zaidi. Sasa zile shillingi miamoja zaidi ndiyo Riba yenyewe.

➡Allaah (Subhaana wa Taala) anatuhimiza kuwa ikiwa mtu anataka kumkopesha mwenzake mwenye shida, basi amkopeshe mkopo mwema bila ya kumuongezea mwenzake dhiki, na kwamba kufanya hivyo ndiyo mali yake mtu inaongezeka baraka itokayo kwa Mola wake, ama unapomkopesha mwenye shida kisha ukachukua faida ya Riba, basi huko ni kumzidishia dhiki mwenzio na pia ni kuiangamiza mali yako na kuiondolea baraka.

Riba hii pia inahusisha ziada juu ya deni kwasababu ya kuakhirisha kulipa pale ambapo mkopaji ameshindwa kulipa kwa wakati ambapo huongezewa kiasi cha ziada cha kulipa kwa kushindwa kulipa deni kwa wakati.


✅Hii pia ni haramu, Kwani hukumu za mdaiwa zipo wazi pindi muda wake unapokwisha. 


Nazo ni amma kumsamehe au kumpa muda zaidi na si kuongeza deni. Allaah(Subhaana wa Taala) anasema

“Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua” 
↪Surat Al-Baqarah Aya ya 280

Ama tukija kufunga mlango wa nyuma wa kula riba katika hadith ya Anas ibn Malik (Radhi za Allah ziwe juu yake) Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amekataza mkopeshaji kupokea zawadi kutoka kwa mkopaji, pia katika hadith nyingine ya Anas ibn Malik katika Sunan al-Bayhaqi Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amekataza mkopeshaji kuchukua chakula au kupanda kipando cha mkopaji kama haikuwa ada yao kabla ya kukopeshana.

Ukweli ni kwamba aina hii ya riba imeshika hatamu katika wakati wetu huu nakuwa moja ya sehemu ya msingi ya uchumi na biashara. 

Mfumo wote wa kifedha umejengwa juu ya riba, kutoka kwenye vyama vya kuweka akiba na kukopa mpaka benki zinazoitwa benki za kibiashara (commercial banks) hujiendesha kwa riba kama chanzo mama cha mapato.

Kutoka kwa Abu Hurayrah: Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amesema “Kwa hakika itakuja zama kwa mwanaadamu ambapo kila mtu atakula riba na kama hatofanya hivyo vumbi lake litamfikia”

↪Imepokelewa na Imaam Abu Dawud na Ibn Majah


                                                            2.RIBA  YA  AL-FADHIL


➡Riba ya Al-Fadhil (kufadhilisha) ni ile ya kubadilishana pesa kwa pesa au chakula kwa chakula na kuchukuwa zaidi.

➡Kwa mfano mtu anapokwenda kubadilisha dhahabu yenye uzito wa gram kumi kwa ajili ya kupata dhahabu nyengine iliyomvutia zaidi, akalipwa badala yake dhahabu yenye uzito wa gram saba. Hiyo inahesabiwa ni Riba. 

➡Inavyotakiwa kwanza mtu aiuze dhahabu ile kwa thamani yake, kisha ainunue dhahabu anayoitaka. 

➡Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amesema; "Msiuze Dirham moja kwa Dirham mbili, kwani nakuogopeeni Riba".
Na akasema; "Dhahabu kwa dhahabu, fedha kwa fedha, ngano kwa ngano, chumvi kwa chumvi, mkono kwa mkono, atakayechukua zaidi au kutaka zaidi, kesha kula Riba" 
↪Imepokelewa na Imaam Ahmad na Al-Bukhariy.

➡Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume Muhammad(Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) akiwa amebeba tende.Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) akamwambia; "Tende hii haipatikani kwetu hapa?" Mtu yule akasema; "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tumebadilishana tende yetu pishi moja kwa pishi mbili za tende hizi". 

➡Mtume Muhammad (Swallah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) akamwambia; "Hiyo ni Riba, zirudishe, kisha uza tende yetu, halafu nunua tende hizi" 
↪Imepokelewa na Imaam Muslim


✅Kwa ujumla ni haramu kuzidisha katika kubadilishana kitu cha jinsi moja. 

➡Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) amebainisha bidhaa sita ambazo ni ngano, dhahabu, fedha, tende, shairi na chumvi ambapo katika kubadilishana bidhaa ya namna moja hubadilshwa kwa bidhaa ya namna hiyohiyo kwa kipimo cha ujazo au uzito ulio sawa bila kuzingatia tofauti ya ubora iliyopo.

➡Mathalan kilo moja ya tende ya daraja ya juu kwa ubora hubadilishwa kwa kilo moja ya tende ya daraja ya chini yenye ubora duni na si vinginevyo. 

➡Au anaehitaji tende za daraja ya juu auze tende zake zenye ubora duni katika soko na atumie thamani hiyo kununua tende za daraja ya juu katika ubora. 

➡Na bidhaa hizi hubadilishwa hapo kwa papo, mkono kwa mkono (spot transaction).

➡Na inaruhusiwa kuzidisha ikiwa vitu vya jinsi mbalimbali. 

Mfano

Mfano kilo mbili za ngano kwa kilo moja ya tende. Lakini hairuhusiwi kuahirisha katika vitu vya aina hii, yaani inatakiwa mkono kwa mkono.

✅Kuharamishwa aina hii ya riba kuna kufunga mlango wa nyuma wa kula riba na aina yoyote ya dhuluma, udanganyifu na hadaa katika kubadilishana bidhaa.


Na  Allaah  anajua  zaidi


➡Mfano umeenda kwa Ally kumkopa Pesa Shilingi 10,000/= na akakuambia


https://ift.tt/2UtMQ2r i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...