Translate

Jumatano, 3 Aprili 2019

Katazo la Wanawake Kutoka Nje huku akiwa amejitia [Ananukia] Manukato

                   Katazo la Wanawake Kutoka Nje huku akiwa amejitia [Ananukia] Manukato


Moja katika madai ya wanawake ni kuwa mtu si vizuri kusikiwa harufu mbaya [majasho]; juu ya kuwa kuna waume ambao hawasikia harufu nzuri za wake zao isipokuwa pale wanapotoka kwenda katika maharusi; katika kulidhibiti hilo huwa wanapotoka kwa kutaka kutimiza mahitajio yao, kwenda shughulini au shughuli zao za kawaida hujitia manukato yenye kuhanikiza, udi, mafuta mazuri, mafuta ya nywele yenye kunukia au mafuta ya kujipaka mwilini yenye kunukia au hata wanapokoga hutumia sabuni zenye kunukia ili wawe na harufu wanapotoka; desturi hii inawapeleka wengine kushikamana nayo hata wanaposaidiwa kupelekwa pahala kwa gari iwe ya kulipa au ya rafiki wa mume [akiwa na huyo mume mwenyewe ndani ya gari] au hata kwenda Misikitini hujimwagia manukato na kusikiwa na kila mtu awe mpita njia, dereva, na kadhalika.

Kwa anayeelewa basi huu ni msiba, na msiba huwa mkubwa zaidi kwa asiyeelewa; kwani jamii yaonyesha kuwa si kuwa iko mbali tu na mafundisho aliyokuja nayo Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), bali jamii imeyatupa mbali na kuyadharau mafundisho na kila lenye kuambatana na mafundisho hayo.

Kutoka kwa bibi Zaynab ath-Thaqafiyyah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:"Atakapo shuhudia mwanamke mmoja wenu Swalah ya 'Ishaa [na katika riwaayah: Msikitini] basi asiguse manukato usiku huo”[Imepokelewa na Muslim, kitabu cha Swalah, mlango wa kutoka wanawake kwenda Misikitini ikiwa haitosababisha fitnah na hali yeye..., Hadiyth namba 678 na namba 679].

Na kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):”Mwanamke yeyote yule ataejifukiza udi [harufu nzuri] basi asishudie pamoja nasi Swalah ya ‘Ishaa ya mwisho” [Imepokelewa na Muslim, kitabu cha Swalah, mlango wa kutoka wanawake kwenda Misikitini ikiwa..., Hadiyth namba680.]

Na kutoka kwa Abu Muusa Al-Ash-‘ariy (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ”Mwanamke yeyote yule ataejitia manukato akapita mbele ya watu ili waipate harufu yake basi huyo ni mzinifu [atakuwa amezini][Imepokelewa na Ahmad katika musnad wake, kitabu Musnad wa watu kumi waliobashiriwa pepo, hadiyth ya Abi Musa Al-Ash-‘ariy (Radhiya Allaahu 'anhu), Hadiyth namba 19272 na 19305; na at-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Adabu, mlango wa yaliyokuja katika yenye kuchukiza kutoka kwa mwanamke ..., Hadiyth namba 2730].

Hadiyth hizi zote dada yangu katika iymaan zinathibitisha uharamu wa kutoka nyumbani kwako hali ya kuwa unanukia, kwani manukato au harufu yake haraka huwafanya wanaume wavutiwe na kupata matamanio ya kutaka kumkaribia aliyejipaka hayo manukato.

Katika kusherehesha neno [huyo ni mzinifu] Wanazuoni wanasema kuwa “Amezini kwa kuwa amesababisha kuzindua matamanio ya wanaume kwa hiyo harufu wanayoipata inayotokana na manukato [au udi] aliyojitia; jambo linalowapelekea kutaka kuelewa nani huyo mwenye kunukia na hilo huwapelekea kumkodolea macho; na mwenye kumtazama huwa amezini [zinaa ya macho], kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Abu Hurayrah(Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:“Ameandikiwa kila mwanaadamu sehemu yake katika zinaa; hakuna njia ya kuiepuka; macho mawili zinaa yake ni kutazama, masikio mawili zinaa yake ni kusikiliza, na ulimi zinaa yake ni kusema, na mkono zinaa yake ni kuunyoosha, na mguu zinaa yake ni hatua zake, na moyo hupata matamanio, na tupu husadikisha au kukadhibisha” [Imepokelewa Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Tafsiyr Qur-aan, Suurat Qul A’uwdhu birabbil Falaq, Hadiyth namba 6152; naMuslim, katika Kitabu cha Qadar, mlango wa imekadiriwa juu ya kila mwanaadam sehemu yake katika zinaa, Hadiyth namba 4808 na namba 4809].

Ni jambo linaloeleweka kuwa kumtazama mwanamke ni katika vitangulizi vya zinaa ya sehemu za siri za wanaume, hivyo ni wajibu kwa kila dada mwenye kuamini Allaah na Siku ya Qiyaamah kutotoka nyumbani kwake isipokuwa kwa haja [dharura] yenye kukubalika na Shariy’ah, na hapo atapohitaji kutoka, basi ahakikishe kuwa anajipamba kwa adabu za kishariy’ah ambazo miongoni mwake ni kuwa amejifunika na kujisitiri vizuri kwa hijabu ya kishariy’ah; na wakati wowote ule ataporudi nyumbani kwake yuko huru kujitia manukato atakavo, kwa sharti kuwa hawatoipata harufu ya manukato yake wanaume wengine wasio kuwa maharimu zake.

 Na  Allaah anajua  zaidi


https://ift.tt/2Vfrfbn i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...