Translate

Ijumaa, 8 Februari 2019

Talaka kwa mwenye Hasira inajuzu?

Swali

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh Sheikh wangu, Pole na Majukumu naona bidii zako kwenye Group kwa kuelimisha Waislamu wenzako na darsa zako kiukweli zinanipa Faida sana Allaah akulipe zaidi

Nina swali moja nauliza kwamba,

Mume alitoa Talaka akiwa na Hasira, Je talaka inasihi...?



Jibu

Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh

Allaahumma Amiin, Allaah atulipe sote ndugu yangu katika Imaani.

Ama kuhusiana na Swali lako ni kwamba Talaka inapita kwa wanazuoni wengi pindi mume mwenye kuitoa akiwa na akili timamu, kwa hiari yake na amebaleghe, lakini akiwa ni mwenda wazimu, mtoto au amelazimishwa basi talaka haipiti.

Sasa tukija kwa talaka ya aliyekasirika (mwenye ghadhabu) lakini yule ambaye hajui kabisa anachosema wala hatambui kinachotoka, talaka huwa haipiti.

Amepokea Ahmad, Abu Dawud, Ibn Maajah na al-Haakim, ambaye ameisahihisha kutoka kwa ‘Aishah (Radhiya Allahu 'Anha) kuwa Mtume (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wasallam)  amesema: “Hakuna talaka wala kuacha huru (mtumwa) katika Aghlaaq”.

Na Aghlaaq imefasiriwa kuwa ni ghadhabu, na pia kutendesha nguvu, na pia imefasiriwa kamauenda wazimu.

Na Ibn Taymiyah amesema kama ilivyonukuliwa katika Zaad al-Ma‘aad: “Hakika yaal-Ighlaaq ni mtu kufunga moyo wake na wala asiwe ni mwenye kukusudia maneno au pia asiwe ni mwenye kujua kama kwamba imefungwa kwake lengo lake na uamuzi wake.

Na inaingia katika hilo talaka ya aliye lazimishwa, na mwenda wazimu, na aliyepoteza akili yake kwa sababu ya vileo (mlevi) au ghadhabu (hasira) na kila ambacho hukukusudia wala huna maarifa nacho kwa ulichosema”.

Na wanachuoni wameigawanyaghadhabu sehemu tatu:

1. Kuwa ile ghadhabu ni mwanzoni wa jambo lake, haibadilishi akili ya mwenye hasira kwa kuwa anakusudia kwa anayosema na anayajua. Na bila shaka kuwa talaka kwa maana hii ya ghadhabu inapita kwa kukubaliwa na wanachuoni wote.

2. Ni ile ambayo ghadhabu inakuwa mwisho na inaharibu akili yake na kumfanya kama mwenda wazimu ambaye hakusudii anayoyasema wala hayajui. Ghadhabu kwa maana hii haipiti kwani yeye na mwenye wazimu ni sawa.

3. Hii ni ghadhabu ambayo ipo katika hali hizo mbili za juu. Anakuwa mkali na anatoka katika ada na ukawaida wake lakini hawi kama mwenda wazimu, ambaye hakusudii anacho sema wala hajui. Na rai ya Jamhuur ni kuwa talaka hii inapita (Abdur-Rahmaan al-Juzayriy, Kitaabul Fiqhi ‘Alal Madhaahib al-Arba‘ah, Mj. 4, uk. 294).

Baada ya kusema haya inatakiwa ifahamike kuwa talaka si kitu cha mchezo na kinatakiwa kitolewe katika hali ya utulivu wa roho na mwili.

Na ndio Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wasallam)akatuusia kuwa tusighadhike, na akalikariri hilo mara kadhaa (Al-Bukhaariy kutoka kwa Abu Hurayrah [Radhiya Allahu 'Anhu]).

Na pia ikiwa tutakasirika nasi tumesimama, basi tukae. Ikiwa itaondoka sawa lau haitaondoka basi jilazeni (Abu Daawuud kutoka kwa Abu Dharr [Radhiya Allahu 'Anhu ])

Hivyo, ni nasaha kwa waume wasiwe ni wenye kutoa haraka talaka kwa wake zao kisha wakawa ni wenye kujuta, kwani hakuna mchezo na talaka.

Na lau talaka hii itapita kwa sababu hatujui hali ya mume wako katika ghadhabu yake itahesabiwa kuwa ni talaka moja na wala sio tatu, hivyo mna uwezo ikiwa mnataka kuishi pamoja kurudiana kabla ya kupita eda bila kufungwa nikaha nyengine.

Ikiwa eda itapita basi itabidi mume ikiwa anamtaka kumrudia mkewe, afuate njia kama ya awali kwa kumposa na kumpatia mahari, kwani hii inakuwa ni ndoa mpya.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 



from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SjaVZv
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...