Translate

Ijumaa, 8 Februari 2019

Inafaa Kutoa Talaka tatu kwa mara moja?

Swali

Naomba kuulza Mwalim mtu anaruhusa ya kumpa talaka 3 kwa Mara moja mkewe? Hilo swali ni mtu kaniulza anatka kujua

Jibu

✅Naam hakika hili ni tatizo kubwa sana kwa jamii zetu za Waislamu katika nchi tofauti kutokana na Ukosefu wa Elimu ya Dini ima kwa Mwanamke au Mwanaume.

➡Hii yote inarudi kwetu sisi na inatokana kwa kupuuza masomo ya Dini yetu tukufu na matatizo haya yataendelea mpaka tutakapoamua kurudi kwa Dini yetu katika kila mambo yetu.

✅Talaka ya aina hii katika sheria inaitwa Twalaqul Bidi‘iy (Talaka ya Kuzuliwa) kwani huwa imekwenda kinyume na sheria tukufu ya Kiislamu. Na hii ni ima kumpatia talaka mke wako akiwa katika damu ya hedhi, nifasi au talaka tatu kwa mara moja au sehemu moja.

✅Wanazuoni wa Kiislamu wametofautiana kama talaka tatu mara moja zinahesabiwa kuwa ni tatu au ni moja.

➡Hii ni kwa sababu kila kundi limetoa ushahidi kwa rai zao.

✅Lakini kauli yenye nguvu zaidi ni kuwa mume anayetoa talaka tatu kwa mara moja inahesabiwa kuwa ni talaka moja lakini atakuwa amefanya makosa na madhambi katika tendo lake hilo na inabidi aombe msamaha.

➡Wakati mmoja Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipashwa habari ya kuwa kuna mtu aliyetowa talaka tatu kwa mara moja.

➡Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikasirika sana na kishaa akasema⤵

“Mnachezea Kitabu cha Allah, nami bado nipo baina yenu”
↪Imepokelewa na Imaam An-Nasai, na akasema Ibn Kathiir kuwa Isnadi yake ni Nzuri.

➡Na alikuwa ‘Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) akiletewa mtu ambaye ametoa talaka tatu kwa mara moja akimpiga viboko (Ibn Abi Shaybah).

➡Na katika mas-ala haya Allah ametuambia kwamba⤵

“T'alaka ni mara mbili”
↪Surat Al-Baqarah Aya ya  229.

✅Hii inamaanisha moja baada ya nyingine na wala siyo kuzitoa kwa wakati mmoja.

➡Sayyid Sabiq katika Fiqhis Sunnah anasema kuwa hii ndiyo iliyokuwa njia iliyofuatwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Abubakr, ‘Umar na Makhalifa wengine (Radhiya Allaahu 'anhum) kabla kubadilishwa.

✅Na hakika inaonyeshwa wazi wazi wakati wa Sheikh Ibn Taymiyah alipotoa rai hii alipingwa sana na wanazuoni wa wakati wake lakini wanazuoni wa sasa wameirudia kauli hiyo ambayo ndiyo yenye nguvu.

Na Allaah anajua zaidi



from fisabilillaah.com http://bit.ly/2DozOc0
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...