Swali: Ni ipi hukumu ya mtu mwenye kuwalaani wazazi wake wawili kwa sababu ya hasira au akawalaani kwa kukusudia? Je, laana hiyo – ni mamoja kwa kukusudia au pais na kukusudia – ina kafara? Je, afanye nini aliyelaani?
Jibu: Kuwalaani wazazi wawili ni katika madhambi makubwa. Kwani imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani yule mwenye kuwalaani wazazi wawili. Ni mamoja kuwalaani huko ikawa ni moja kwa moja au mtu yeye ndiye amesababisha. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa:
“Hivi kweli mtu atawalaani wazazi wake wawili?” Akajibu: “Ndio. Ni pale ambapo atamtusi baba wa mwingine na yeye amtukanie baba yake na amtukanie mama yake na yeye amtukanie mama yake.”
Kwa hivyo kuwatukana wazazi wawili – ni mamoja mtu amefanya hivo moja kwa moja au amesababisha – ni dhambi kubwa. Hakuna tofauti hayo yametokea pasi na sababu au kwa sababu ya hasira. Isipokuwa kuhusiana na hasira mtu hasira ikimfikisha kiwango cha kwamba hajui kile anachokisema, katika hali hiyo hana dhambi. Kwa sababu hakitambui anachokisema. Allaah anamlipa mja kwa kile anachokitambua na si kwa kile asichokitambua. Pamoja na kwamba inatakiwa kwa mtu pale anapokuwa na hasira au kama yeye ni mwenye kushikwa na hasira haraka, basi afanye sababu zinazomwondosha katika hali hiyo au kumpunguzia. Kwa sababu kuna mtu alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuusie ambapo akamwambia:
“Usikasirike!”
Akakariri ausiwe akamwambia:
“Usikasirike!”
Mtu akihisi hasira basi aombe kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa na atawadhe. Kwani hayo ni miongoni mwa sababu zinazoondosha hasira. Miongoni mwa sababu vilevile mtu aondoke na aende mbali na hasimu wake ili kusitokee kitu katika madhara.
Swali: Upande wa tawbah inakubaliwa tawbah yake?
Jibu: Kuhusiana na tawbah yuko na tawbah. Hakuna dhambi yoyote isipokuwa ikiwa na tawbah. Amesema (Tabaarak wa Ta´ala):
قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
“Sema: “Enyi waja Wangu ambao mmepindukia juu ya nasfi zenu: “Msikate tamaa na rehema za Allaah. Kwani hakika anasamehe madhambi yote. Kwani hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (39:53)
Lakini ilipokuwa dhambi hii inahusiana na haki ya kiumbe basi ili tawbah iweze kusili basi ni lazima amuombe msamaha yule aliyemfanyia vibaya ili tawbah yake iweze kutimia.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2GdcSQ9
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni