Swali: Sisi tunaishi kwenye kijiji chenye milima na kinachotisha sana na mara nyingi tunatumia wanyama kama vipando kwenda huku na kule. Mfano wa wanyama hao ni ngamia, punda, nyumbu na wengineo. Ni mamoja tunapoenda masomoni ambayo yako mbali kidogo na kijiji chetu kwa takriban 10 km. Tunawapiga kipigo cha kuumiza ili waweze kutembea na wachapue kwenda masomoni. Ni ipi hukumu ya kuwapiga wanyama ili wachapue na masafa yawe mafupi au kumpiga kwa kukusudia? Kwa sababu nimesoma Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba wanyama watamlipiza kisasi mtu siku ya Qiyaamah. Tunaomba faida na Allaah akujaze kheri.
Jibu: Hapana shaka kwamba wanyama wana roho na hisia. Wanaumia na wanahisi ugumu na uzito kwa yale yenye kushinda uwezo wao. Hivyo haifai kwa muislamu kumbebesha mnyama asichokiweza. Ni mamoja kitu hicho kiwe kinabebwa mgongoni mwake, kitu anachokibeba kwenda mahali fulani asipoweza au hali nyinginezo ambazo hawezi.
Kuhusu kumpiga inafaa wakati wa haja kwa sharti asimuumize. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Jaabir kuhusu kisa cha ngamia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikutana naye na ndani yake imetajwa kwamba alikuwa akimpiga ngamia. Kimsingi ni kwamba kuwapiga wanyama, midhali mtu hawaumizi, inafaa. Dalili katika Sunnah ni Hadiyth ya Jaabir. Ama ikiwa ni pasi na haja, ikawa ni kipigo cha kuumiza au ikawa ni kipigo kitachomfikisha mnyama katika jambo zito kwake, hapo haitofaa.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2TosOCJ
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni