Translate

Jumatano, 3 Aprili 2019

Katazo la Wanawake kufunga Sawm ya Sunnah bila Idhini ya Mume

        Katazo la Wanawake kufunga Sawm ya Sunnah bila Idhini ya Mume

Wanawake wengi huwa wanapendelea kufunga Swawm za Sunnah; na wakati mwingine kwa pupa zao za upendaji wao wa mambo ya kheri na kutaka kujikumbia fadhila zilizofungamana na Swawm za Sunnah utawaona wanakimbilia kutekeleza Swawm za Sunnah au hata kutaka kuzitanguliza kabla ya kutimiza za waajib; wakisahau kuwa Swawm ya wajibu [fardhi] ni deni na isipotekelezwa huwa ni kosa kinyume na utekelezaji wa Swawm ya Sunnah ambayo ni jambo la mtu kujipendekeza kwa Muumba wake.  

Kwa hali hii huwapelekea wengi miongoni mwa dada zangu katika iymaan kujifungia Swawm ya Sunnah kwa kutafuta fadhila na kujikurubisha kwa Allaah bila ya kuelewa kuwa huyo wanayetaka kujikurubisha Kwake na kwa kuwapatia Fadhila Zake, Amewataka kwa kupitia Mjumbe Wake(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wawe na hadhari ya kutofunga Swawm yoyote ile ya Sunnah bila idhini ya waume zao.

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:“Asifunge mwanamke [Swawm ya Sunnah] na huku mumewe yuko pamoja nae isipokuwa kwa idhini yake huyo mume na wala asimruhusu mtu katika nyumba ikiwa mumewe yuko isipokuwa kwa idhini yake huyo mume [Imepokelewa na Al-Bukhaariy,kitabu cha Nikaah, mlango wa Swamw ya Sunnah ya mwanamke kwa idhini ya mumewe, Hadiyth namba 4820; na katika Kitabu cha Tafsiri Qur aan, Suuratul Qul A’uwdhu birabbil Falaq, Hadiyth namba 4823; na Muslim, katika Kitabu cha Zakaah, mlango wa atachotoa mtumishi katika mali ya tajiri wake, Hadiyth namba 1710].

Imaam An-Nawawiy amesema: Hii inakusudiwa Swawm ya Sunnah na Swawm zote zisizokuwa za nyakati maalumu, na hili katazo la uharamu liko wazi, na sababu yake ni kuwa mume ana haki ya kustarehe na mkewe katika siku zote za wiki, na haki hii ni waajib ulio wa haraka; hivyo haiwezi ikaondoka [ikaporomoka] au kudondoshwa kwa Sunnah wala kwa jambo la waajib lisilo la haraka.
Na kauli yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “... na huku mumewe yuko pamoja nae na maana kama kama mume atakuwa safarini na mke yuko nyumbani, mke huyo atakuwa huru kufunga Swawm ya Sunnah.

Na   Allaah  anajua  zaidi


https://ift.tt/2CP9dp4 i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...