Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah: 281 : Aayah Ya Mwisho Kuteremshwa
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾
281. Na iogopeni Siku mtakayorejeshwa ndani yake kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa
Mafunzo:
Wengi kati ya ‘Ulamaa wamekiri kwamba hii ni Aayah ya mwisho kuteremshwa. Na miongoni mwa Salaf waliokiri ni Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), na Sa’iyd bin Jubayr (رحمه الله) kwa Riwayaah mbalimbali kwamba baada kuteremshwa Aayah hii yakapatika masiku kadhaa kisha akafariki Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) [An-Nasaaiy – Tafsiyr Ibn Kathiyr].
Na Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema: “Hii ni Aayah ya mwisho iliyoteremshwa katika Qur-aan, na ikafanywa ni hatima ya hukmu na maamrisho na makatazo kwa sababu humo mna ahadi za matendo ya kheri, na tisho la matendo maovu, na kwamba anayejua kwamba yeye atarejeshwa kwa Allaah ili Amlipe kwa dogo na kubwa (aliyoyatenda) na yaliyodhahiri na ya siri na kwamba Allaah Hatomdhulumu chembe ya hardali (au atomu), basi itamwajibika awe na raghbah (utashi, matumaini) na khofu...”
from Alhidaaya.com http://bit.ly/2TYcI2n
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni