Translate

Jumanne, 2 Aprili 2019

02. Kijana ambaye anaweza kuyapambanua mambo aamrishwe kufunga?

Swali 2: Kijana ambaye anaweza kuyapambanua mambo aamrishwe kufunga? Je, itasihi kwake iwapo atabaleghe katikati ya mchana?

Jibu: Kumetangulia katika jibu la swali la kwanza ya kwamba mtoto wa kiume na wa kike wakifikisha miaka saba na zaidi basi wanatakiwa kuamrishwa kufunga ili waizowee. Ni lazima kwa wasimamizi wao kuwaamrisha kama wanavyowaamrisha kuswali. Wakishabaleghe basi watalazimika kufunga. Wakibaleghe katikati ya mchana basi siku hiyo itasihi kwao. Tukadirie kuwa mvulana amefikisha miaka kumi na tano wakati wa kupindukia kwa jua ilihali amefunga basi siku hiyo itasihi kwake. Sehemu ya mwanzo ya mchana itakuwa ni Sunnah kwake na sehemu ya mwisho ya mchana itakuwa ni faradhi. Hapo ni pale ambapo alikuwa hakubaleghe kabla ya hapo kwa kuota nywele kwenye makwapa au kutokwa na manii kwa matamanio. Vilevile inahusiana na mtoto wa kike. Wawili hao wana hukumu moja. Pamoja na kwamba kuna jambo la nne linalozidi kwa mtoto wa kike ambalo hubaleghe kwalo. Nalo ni kupata hedhi.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2Uhc1Gw
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...