Swali 14: Ni jambo linalojulikana ya kwamba kulingania katika dini ya Allaah ni kitu kinachohitajia elimu ya Kishari´ah. Je, kinachozingatiwa ni kuhifadhi Qur-aan na Sunnah? Inatosheleza elimu ambayo mtu anasoma kwenye masomo na kwenye vyuo vikuu?
Jibu: Elimu inahusiana na mtu kuhifadhi maandiko na kuelewa maana yake. Haitoshelezi kuhifadhi maandiko peke yake. Haitoshelezi kwa mtu hifadhi maandiko ya Qur-aan na Sunnah. Isitoshe ni lazima kwa mtu kufahamu maana yake sahihi. Kuhifadhi peke yake pasina kuelewa maana yake haimstahikii yeyote kulingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall).
Ama yale yanayosomwa masomoni, yanatosheleza ikiwa yanahusiana na kuhifadhi maandiko na kufahamu maana yake. Ikiwa inahusiana na kuhifadhi maandiko peke yake pasina kuelewa maana yake, hili halistahikii kulingania. Hata hivyo inawezekana kuwahifadhisha wanafunzi maandiko kabla ya kuwafafanulia maana yake au kuwasomea nayo na wakasikiliza.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2DjY4Ms
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni