أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Anfaal: 75
075- Na Wale Walioamini Baada Na Wakahajiri Na Wakafanya Jihaad Pamoja Nanyi Basi Hao…
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالَّذِينَ آمَنُوا مِن بَعْدُ وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا مَعَكُمْ فَأُولَـٰئِكَ مِنكُمْ ۚ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿٧٥﴾
75. Na wale walioamini baada (ya hijra) na wakahajiri na wakafanya jihaad pamoja nanyi; basi hao ni miongoni mwenu. Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika shariy’ah ya Allaah. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu.
Sababun-Nuzuwl:
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaunga undugu Maswahaba wakawa wanarithiana mpaka ilipoteremka: “Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe.” Wakaacha kurithiana wakawa wanarithiana kwa uhusiano wa damu. [Atw-Twabaraaniy, na amesema Al-Haythamiy katika Majma’u Az-Zawaaid (7/28) Watu wake ni Swahiyh, na ameipokea Ibn Abiy Haatim (4/25) Hadiyth ya Az-Zubayr bin Al-‘Awwaam (4/24) na ameipokea Ibn Jariyr (10/58)].
from Alhidaaya.com http://bit.ly/2Q6P8OL
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni